Kabendera apandishwa kizimbani afunguliwa mashtaka matatu

Kabendera apandishwa kizimbani afunguliwa mashtaka matatu

05 August 2019 Monday 13:59
Kabendera apandishwa kizimbani afunguliwa mashtaka matatu

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mwandishi wa habari nchini, Erick Kabendera amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na  kusomewa mashtaka matatu tofauti.

Makosa hayo ni  kujihusisha na genge la uhalifu, uhujumu uchumi kwa kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja na utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya milioni mia moja na sabini.

Awali Julai 30 baada ya kukamatwa kwake Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ilidai kumkamata kwa ajili ya mahojiano ya uraia wake

Lakini leo Agosti 5, 2019 kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa mahakamani, Kabendera anadaiwa kutekeleza hayo yote baina ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar Es Salaam  kwa kushirikiana wa watu ambao hawakuwepo mahakamani leo.

Makosa yote hayana dhamana. Mawakili wake wameondoa ombi la dhamana kutokana na mashtaka hayo mapya.

Julai 29 majira ya jioni Erick Kabendera alichukuliwa kwa nguvu kutoka kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam eneo la Mbweni. Kabendera anaandikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania,.

Updated: 05.08.2019 14:07
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.