Kampuni tatu za usafirishaji kunyimwa leseni

Kampuni tatu za usafirishaji kunyimwa leseni

30 June 2019 Sunday 12:17
Kampuni tatu za usafirishaji kunyimwa leseni

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, ametishia kuzinyima leseni kampuni tatu zilizoomba leseni kwa ajili ya kuendesha bandari kavu(ICDS) kwa tuhuma za kuhamasisha mgomo wa malori bandarini.

Wamiliki wa kampuni hizo wanatuhumiwa kuhamasisha madereva wa malori yanayotoa mizigo bandarini kufanya mgomo kuanzia Juni 29, 2019 mchana hadi usiku kwa lengo la kuondolewa kwa mizani ya kupima uzito wa magari hayo kabla ya kuanza safari zake kwa njia ya barabara.

Amesema hayo, alipofanya ziara ya kukagua mizani hizo kuona kama inasababisha msongamano kama ilivyodaiwa na baadhi ya wafanyabiashara hao na kubaini kuwa lori moja linachukua sekunde 55 hadi dakika moja kupimwa uzito.

"Nimekuja nione kama kweli hizi mizani zinasababisha msongamano, lakini nimekuta si kweli kwa sababu kuna mizani miwili na yote ni mizima na wanatumia si chini ya dakika moja kupima na kuondoka eneo hili," alisema Kamwelwe na kuongeza;

"Sasa nimeshabaini waliohusika kufanya mgomo huu ni kampuni tatu ikiwamo PrimeFuel ambao tunawaita ni 'Wahaini' kwa sababu lengo lao ni kukwamisha miradi ya Serikali na waliomba leseni za ICDS sasa tutawaonyesha kama sisi ni Serikali na walichofanya si sahihi"

Leseni za wafanyabiashara wa ICDS zinatoka Julai 17 na wafanyabishara waliohusika kufanya hujuma hizo hawatapatiwa leseni zao kwa sababu wanakwamisha juhudi za Rais John Magufuli.

Updated: 30.06.2019 12:28
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Yassin Sadik 2019-06-30 16:14:02

Than 4 well researched stories