Kauli 'tata' ya waziri Kabudi yaishtua serikali

Kauli 'tata' ya waziri Kabudi yaishtua serikali

11 July 2019 Thursday 15:41
Kauli 'tata' ya waziri Kabudi yaishtua serikali

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
SUALA la kupotea kwa mwandishi Azory Gwanda limezidi kuongeza SINTOFAHAMU na  sasa Serikali imesema hadi sasa hakuna uthibitisho kuwa mwandishi huyo yupo hai au amefariki.

Lakini Julai 10, 2019 katika mahojiano na BBC katika kipindi cha FOCUS ON AFRICA mjini London waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi amekaririwa akisema Gwanda 'alitoweka na kufariki' Pia alisema visa vya watu kutoweka vimesababisha uchungu mwingi nchini. 

Taarifa ya leo Julai 11, 2019 ya  msemaji mkuu wa serikali, Dk Hassan Abas inaeleza "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki. Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuchunguza tukio hilo na matukio mengine yaliyotokea katika machafuko ya Kibiti, Pwani yaliyosababisha ama watu kadhaa kupoteza maisha au kupotea."

Pia taarifa iliyotolewa  leo na profesa Kabudi inaeleza; "Nimepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu kimakosa mahojiano yangu kwenye kipindi cha BBC FOCUS ON AFRICA zikidai kuwa nimethibitisha kwamba mwanahabari Azory Gwanda amefariki dunia."

"Hii sio tafsiri sahihi kuhusu kile nilichokisema. Katika mahojiano hayo nilieleza kuwa tukio lililotokea Kibiti lilikuwa ni la kuhuzunisha na wapo watanzania waliouwawa na wengine kupotea. SIKUTHIBITISHA kuwa Azory Gwanda amefariki."

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na kampuni ya magazeti ya mwananchi, mwanahabari huyo wa kujitegemea alitoweka Novemba 21, 2017.

Gwanda alikuwa anaishi na kuripoti kutoka mji wa Kibiti wilayani Rufiji mkoani Pwani, ambao upo kilomita takriban 130 kusini mwa jiji la  Dar es Salaam.

Gwanda ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa kuripoti kwa kina juu ya mfululizo wa mauaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana yaliyowalenga polisi na viongozi wa mji huo na kuzua hofu kubwa.

Mke wake Anna Pinoni alisema watu wapatao wanne wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua Gwanda kutoka katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa.

Anasema pia aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kwamba inawezekana waliipekua nyumba yao.

Azory aliwasiliana na ofisi za Mwananchi mara ya mwisho  Novemba 20 kwa majukumu ya kikazi.

Mjadala kuhusu kutoweka kwa mwandishi huyo wa uchunguzi ulitanda kila sehemu nchini humo huku waziri wa habari wa Tanzania akiliambia bunge kwamba kesi yake ni hafifu kwa kuwa alipotea eneo ambalo mamia ya Watanzania walipotea.

PICHANI: Msemaji mkuu wa serikali na mkurugenzi wa idara ya habari Maelezo, Dk Hassan Abas ambaye pia 

Updated: 12.07.2019 08:40
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.