Kesho kupatwa kwa mwezi

Kesho kupatwa kwa mwezi

15 July 2019 Monday 12:08
Kesho kupatwa kwa mwezi

Na Dk Noorali T Jiwaji

Mwezi utapatwa kiasi usiku wa Jumanne, Julai 16, 2019.  Kwa maeneo yetu ya dunia, yaani Afrika, kupatwa kungine wa kuangaliwa kwa urahisi hakuta tokea kwa miaka 10 ijayo. 

Kupatwa kwa Mwezi mara ya mwisho kulitokea mwaka jana tarehe 27 Julai, 2019.  Baada ya miaka kumi Desemba 20, 2029 kutatokea kupatwa kamili kwa Mwezi ambao utaweza kuangaliwa kwa muda mzuri wa watu kuwa macho. 

Kwa hiyo kupatwa  siku ya Jumanne  ni nafasi nzuri sana kwenda kushuhudia Mwezi ukimegwa na kiza cheusi na kuona jinsi kupatwa kunaendelea angani.  Julai pia ni wakati ambao mara nyingi anga linakuwa wazi bila mawingu. 

Maelezo ya kupatwa:

⦁ Kupatwa kutaonekana usiku wa Jumanne tarehe 16 Julai 2019

⦁ Kiasi cha Mwezi kufunikwa: Asilimia 65 ya sura ya Mwezi hautaonekana

⦁ Jumla ya muda wote wa kupatwa: Masaa 5 dakika 34

⦁ Kiza chepesi kuanza kufunika Mwezi (amabao siyo rahisi kutambua): Jul 16 saa 3:44 usiku

⦁ Kupatwa kiasi kunaaza (ukingo wa Mwezi utaanza kumegwa): Jul 16 saa 5:02 usiku

⦁ Kupatwa zaidi kabisa: July 17 saa 6:31 mara baada ya saa 6 usiku

⦁ Kupatwa kisai kutaisha (yaani uweusi utatoka na Mwezi kuwa mviringo): July 17 saa 2:00 usiku wa manane

⦁ Kiza chepesi kitatoka: Jul 17 saa 9:18 usiku wa manane

⦁ Muda wa uweusi kushamiri kwa jumla ya masaa matatu kuanzia saa 5 usiku hadi saa 2 usiku wa manane.

Kupatwa hutokea kutokana na Mwezi kuzunguka Dunia, na Jua, Mwezi na Dunia kujipanga mstari.  Wakati wa kupatwa kwa Mwezi magimba hujipanga: Jua-Dunia-Mwezi katika mstari kwa hiyo kuvuli cha Dunia kinaweza kuangukia Mwezini.  Uelewe kuwa violwa hivi havijipangi kila mara kila mwezi kwa vile mzingo wa Mwezi umeinama kwa kiasi kidogo na mzingo wa Dunia kuzunguka Jua.

Wakati wa kupatwa KIASI kwa Mwezi mstari huwa HAUJANYOOKA moja kwa moja.  Ila wakati wa kupatwa KAMLIFU, mstari HUNYOOKA KABISA.  Jumanne ijayo tarehe 16 Julai, 2019 Mwezi utapatwa kiasi kwa hiyo mstari wa Jua-Dunia-Mwezi hautakuwa umenyooka moja kwa moja.

Kupatwa kwa Mwezi huonekana katika maeneo mengi ya Dunia kwa vile kivuli cha Dunia linakuwa kubwa la kuweza kufunika Mwezi kwa muda mrefu wa karibu masaa matatu.  Kupatwa Jumanne hii unatokea anga 

Kupatwa kwa Mwezi pia hutokea wakati wa mbalamwezi Mwezi ukiwa mpevu kwa hiyo tarehe 16 Julai ni siku ya Mwezi mpevu na utakuwa unang’aa vikali kupatwa kutapoanza saa 4 kasoro robu usiku.

Mwezi utaanza kwanza kufunikwa na kivuli chepesi kabisa kuanzia saa 3:44 usiku.  Wakati huu si rahisi kutambua mfifio wa Mwezi kutokana na kivuli chepesi, ila kwa vile tunategemea Jumanne anga litakuwa wazi kabisa bila mawingu unweza kujaribu kuangali kiasi fulani kwa Mwezi kufifia mwanga wake.

Kuanzia saa 5:02 usiku, utaona kingo ya kaskazini magharibi ya Mwezi ukianza kumegwa na kivuli cheusi cha Dunia.  Hii itaenedelea kwa saa moja na nusu hivi wakati kivuli cheusi kikisogea juu y asura ya Mwezi pole pole hadi upande wa kaskazini wa Mwezi utafunikwa kwa asilimia 65. Hapo ndiyo kupatwa kukubwa kabisa utakatotokea saa 12: 31 usiku.

Baada ya kiasi kikubwa kabisa cha asilimia 65 ya Mwezi kupatwa, kivuli cheusi kitaanza kuserereka upande wa kusini mashariki wa Mwezi hadi saa nane usiku wa manane ambapo kivuli cheusi kitakuwa kimetoka kabisa na kivuli chepesi kitaenea tena sura yote ya Mwezi.  Kivuli chepesi hiki kitakuwa ngumu kutambua kwa vile hata kama anga liko wazi hautaweza kulinganisha na mng’ao mkali wa Mwezi ukiwa bila kivuli.  Kupatwa kote kutaisha baada saa moja na nusu nyingine hadi saa 9:18 alfajiri

Ujaribu sana kutafuta nafasi na hata kukosa usingizi kidogo ili uweze kuangalia uhalisi wa Mwezi kusogea pole pole ndani ya kivuli cha Dunia katika masaa machache wakati kupatwa kunaendelea.  Hautapata nafasi nzuri kiasi hiki wa kuona kupatwa kote kwa Mwezi kwa miaka 10 ijayo kwa hiyo  usipoteze nafasi hii. 

Updated: 15.07.2019 12:17
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.