Kesi Shamim Mwasha na Mumewe yasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu

Kesi Shamim Mwasha na Mumewe yasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu

24 June 2019 Monday 15:04
Kesi Shamim Mwasha na Mumewe yasubiri ripoti ya Mkemia Mkuu

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

UPANDE wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa inasubiri ripoti ya kielelezo kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride inayomkabili Shamim Mwasha (41) na mumewe, Abdul Nsembo(45).

Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi, Kelvin Mhina wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Wankyo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo anaomba ahirisho la kesi hiyo wakati wakisubiri majibu ya kielelezo kutoka kwa Mkemia Mkuu.

Hata upande wa utetezi umeomba kupewa taarifa kuhusu kukamilika kwa ripoti hiyo.

Katika majibu yake Wakili Wankyo ameutaka upande wa utetezi wawe wavumilivu kwa sababu yeye si msemaji wa Ofisi ya Mkemia Mkuu.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 8, 2019. Washtakiwa wamerudishwa rumande.

Washtakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei 1,2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.