Kesi wanafunzi wanaodaiwa kusambaza picha rais Magufuli kuvaa hijabu yaunguruma

Kesi wanafunzi wanaodaiwa kusambaza picha rais Magufuli kuvaa hijabu yaunguruma

11 July 2019 Thursday 16:33
Kesi wanafunzi wanaodaiwa kusambaza picha rais Magufuli kuvaa hijabu yaunguruma

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Askari   kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mtandao, Anakreti Telesphory (32) ameileza  Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam jinsi walivyowahoji wanafunzi watatu wa Chuo Kikuu cha Kampala na kukiri kusamba kwenye mitandao ya WhatsApp picha inayomuonyesha rais John Magufuli akiwa amevaa Hijabu.

Wanafunzi hao  ni Amenitha  Konga (19),Mariam Twelve(20) na Agnes Gabriel (21) wote wanatetewa na wakili Alphonce Nachipyangu.

Shahidi huyo watatu wa upande wa mashtaka aliyaeleza hayo  leo Julai 11, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi,Catherine Kihoja na wakili wa serikali,Grace Lwila katika kesi ya jinai namba 65 ya mwaka 2016.

Akitoa ushahidi katika kesi hiyo, Telesphory alieleza kuwa majukumu yake ni kufanya doria mitandaoni na kuchambua data za kielektroniki.

Alidai kuwa Juni 13,2016 akiwa ofisini kwake maeneo ya Posta alipewa maelekezo na Inspekta Beatrice ya kwenda katika chuo kikuu cha Kampala kuna mshtakiwa ametuma Picha ya rais akiwa amevaa Hijabu katika grupu la WhatsApp lijulikanalo Human Resource Menagement.

"Tulikwenda hadi chuoni hapo tukaonana na mlezi wa mwanafunzi aitwaye Herma Frank tukamueleza shida yetu kuwa tunawahitaji wanafunzi hao, alikiri kuwa wapo akatuitia" alieleza shahidi huyo.

Alidai kuwa baada ya wanafunzi hao kuitwa alifanya mahojiano na Amenitha ambaye alikiri kuifahamu Picha hiyo inayomuonyesha rais Magufuli amevaa Hijabu na kwamba  aliituma katika grupu la WhatsApp la Human Resource Menagement.

Alipoulizwa alitoa wapi,alieleza  kuwa Picha hiyo ilitumwa katika grupu la whatsapp la  Empire na rafiki yake ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake Maria Twelve.

Telesphory akiendelea kutoa ushahidi alidai kuwa walimuhoji MariamTweve ni wapi alitoa Picha hiyo na kuituma katika group la WhatsApp la Empire  naye alikiri kuifahamu na kwamba aliipata katika grupu la WhatsApp la Business Administration na kwamba ilitumwa humo na Agnes Gabriel.

Telesphory aliendelea kueleza kuwa baada ya hapo walimfanyia mahojiano Agnes naye alikiri kuitambua Picha hiyo na kueleza kuwa ilitumwa katika grupu la WhatsApp la St. Mary's Ulete lakini alishindwa kukumbuka nani aliituma kwenye grupu hilo.

Aliendelea kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo, Telesphory alidai kuwa baada ya kufanya mahojiano hayo walijaza hati za kushikilia Mali ya kila mtuhumiwa kwa ajili ya kushikilia simu zao na laini na kisha wakasaini na mlezi wa mwanafunzi Herma  Frank naye alisaini kama shahidi.

Alibainisha kuwa mahojiano hayo waliyafanya wakiwa katika chuo hicho kikuu cha Kampala baada ya kujitambulisha na kuwa fahamisha watuhuma haki zao za msingi na kwamba baada ya hapo waliwapeleka polisi kati.

Baada ya kutolewa kwa ushahidi huo, wakili Alphonce anayewatetea washtakiwa hao alimuhoji shahidi kama ifuatavyo.

Wakili Alphonce: moja ya Kazi yenu ni kufanya doria mitandaoni mnaifanyaje?

Shahidi Telesphory: Tunaifanya kwa kutumia vifaa vya kitaalamu ambavyo sisi kama askari wapelelezi kuna vitu huwa  tunavitafuta katika mitandao yote ya kijamii na doria hii aina tofauti na ile ya mitaani.

Wakili Alphonce: wewe unafahamu shtaka lililopo mahakamani ni nini?

Shahidi Telesphory: Tuhuma za kusambaza Picha ya rais akiwa amevalishwa Hijabu.

Wakili Alphonce: Wewe umewahi kuziona  Picha zote za rais? 

Shahidi Telesphory:Hapana

Wakili Alphonce: Kama wewe hujawahi kuziona Picha zote za rais unasemaje hii kitu ni kosa?

Shahidi Telesphory: Kwa Picha za rais ninazozijua hii ilinistaajabisha kwa  kuona amevalishwa Hijabu.

Wakili Alphonce: Kama hujawahi kuziona unasemaje siyo yeye.

Shahidi Telesphory: Nimetuhumu hiyo Picha kwa kutazama na kuona hiyo Picha ni ya rais.

Katika kesi hiyo washtakiwa hao, mshtakiwa mwingine ni Anene Mwansasu (23) hana kazi ambapo kwa pamoja wanadaiwa kuwa Juni 9,2016 ndani ya jiji la Dar es Salaam walichapisha taarifa ya uongo kupitia mfumo wa kompyuta.

Kwa sambaza kwenye mtandao wa WhatsApp picha ikionyesha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli akiwa amevaa hijabu vazi ambapo huvaliwa na wanawake wa dini ya kiislamu jambo ambalo si kweli.

Hakimu Kihoja ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 22 na 23, mwaka huu na kuuamuru upande wa mashtaka kupeleka  mashahidi wa kutosha ili kesi iweze kumalizika mapema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.