Kesi ya Shamim, mumewe yaendelea kupigwa danadana

Nsembo na Shamimu wakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin, kinyume cha sheria.

Kesi ya Shamim, mumewe yaendelea kupigwa danadana

Nsembo na Shamimu wakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin, kinyume cha sheria.

27 May 2019 Monday 15:05
Kesi ya Shamim, mumewe yaendelea kupigwa danadana

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

UPANDE wa Utetezi katika kesi  ya uhujumu uchumi inayomkabili, mfanyabiashara, Abdul Nsembo maarufu Abdulkandida(45)na mkewe, Shamim Mwasha(41) umeomba upande wa mashtaka kuhakikisha kuwa wanakamilisha upelelezi kwa wakati, ili kesi hiyo iweze kuendelea na hatua nyingine.

Nsembo na Shamimu wakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin, kinyume cha sheria.

Wakili wa utetezi, Hajra Mungula na Charles Kisoka, wametoa ombi hilo, leo Mei 27, 2019, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Ombi hilo limetolewa mbele ya Hakimu Mkaza Mfawidhi, Kelvin Mhina, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

" Kwa kuwa kesi hii haina dhamana na wateja wetu wanaendelea kusota rumande, tunaomba upande wa mashtaka wajitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati ili kesi hii iweze kuendelea kwa hatua nyingine " alidai Kisoka.

Awali, wakili wa Serikali, Simon Wankyo, alidai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hakimu Mhina, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Kwa mujibu  wa hati ya mashtaka, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 36/2019.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 36/2019, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kusafirisha  dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gram 232.70, wakati wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo, Mei mosi, 2019 katika eneo la Mbezi Beach, Jijini Dar Es Salaam.

Kwa mara  ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa Kisutu, Mei 13, 2019.

Updated: 27.05.2019 15:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.