Kesi ya uchochezi ya Zitto Kabwe yapingwa 'danadana'

Kesi ya uchochezi ya Zitto Kabwe yapingwa 'danadana'

12 September 2019 Thursday 11:29
Kesi ya uchochezi ya Zitto Kabwe yapingwa 'danadana'

Na mwandihi wetu, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Septemba 12, 2019 imeahirsha kesi ya uchochezi inayomkabili kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 7, 8 na 9 2019 kwa sababu shahidi wa upande wa mashtaka ameshindwa kufika mahakamani. Kesi hiyo yenye mashahidi 15 ilianza kuunguruma Januari 29, 2019

Zitto ambaye pia ni mbunge wa kigoma mjini kupitia ACT Wazalendo, anadaiwa kuwa Oktoba 28, 2018 maeneo ya Kijitonyama wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, aliitisha mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho kwa lengo la kuleta chuki kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kwamba kinyume na sheria alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi.

Anadaiwa kutamka kuwa; “watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya Nguruka mkoani Kigoma, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua.”

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.