Kigwangalla: Tulikosea sanamu la Nyerere

Kigwangalla: Tulikosea sanamu la Nyerere

11 July 2019 Thursday 10:19
Kigwangalla: Tulikosea sanamu la Nyerere

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam 
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla ameomba kupewa muda ili kurekebIsha mfano wa sanamu ambalo lilichongwa kuashiria kuwa ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ambalo hivi karibuni lilizua mjadala mkubwa hususani kwenye mitandao ya kijamii.

Julai 9, 2019 katika uzinduzi wa hifadhi ya Burigi-Chato iliyoko Wilaya Chato mkoani Geita Waziri Kigwangalla, alimkabidhi Rais Magufuli mfano wa sanamu la Mwalimu Nyerere, huku watu mbalimbali wakidai sanamu hilo halina uhalisia na Mwalimu Nyerere.

Leo Julai 11, 2019 waziri huyo amesema "Baba wa Taifa alitoa tamko la kwanza la Uhifadhi nchini, ambalo ndiyo dira yetu, tuache dhihaka kwa sababu hakuna aliyefanya kazi ile kwa kusudi hilo, tumesema linashughulikiwa tunaomba mtuamini, mtupe muda turekebishe. Wewe ni malaika. Uko perfect. Huwa hukosei"

"Kilichonifurahisha ni kuwa kizazi cha vijana wa kisasa, bado kinamkumbuka vizuri Baba wa Taifa, kinamuenzi na kumheshimu sana, ndiyo maana wanaikumbuka taswira yake, tutatumia vizuri zaidi wataalamu wetu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kabla ya kuitumia" ameongeza Kigwangalla

Julai 9, 2019 kwenye uzinduzi wa hifadhi ya Burigi-Chato Waziri Kigwangalla pia  alimkabidhi rais Magufuli tuzo maalum ambayo hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilishinda kwa kuwa hifadhi bora barani Afrika.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.