Kisena, mkewe waendelea kusota rumande

Kisena, mkewe waendelea kusota rumande

28 May 2019 Tuesday 13:57
Kisena, mkewe waendelea kusota rumande


Na mwandishi wetu, Dar es salaam
UPANDE wa Utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam Udart, Robert Kisena(46),mkewe Frorencia Mshauri Membe (43) na wenzao watatu wameuomba upande wa mashtaka iwaeleze ni lini watakuwa wamekamilisha  upelelezi .


Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na Chen Shi (32).


Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa Serikali,Wankyo Simon kuieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi bado haujakamilika hivyo wameomba tarehe nyingine ya kutajwa.
"Hii kesi ndiyo kwanza ina mwezi mmoja tangu iunganishwe hivyo ina sehemu nyingi inafanyiwa upelelezi hivyo hatuwezi kusema ni lini au mwezi gani utakuwa umekamilika tutakuwa hatutendi haki kwa wenzetu," amedai Simon.


Upande wa Utetezi,wakili Kanzungu amedai kuwa upande wa mashtaka wanatakiwa kuieleze mahakama upelelezi umefikia wapi."Tunaomba upelezi ukamilike kwa haraka ili shauri kumalizika haraka,"alidai Kazungu.


Hakimu Mkazi Mwandamizi,Augustine Rwizile aliahirisha shauri hilo hadi Juni 6,2019 itakapotajwa tena na washtakiwa wamerudishwa rumande.


Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi mwaka 2011 na Mei 31,2018 katika maeneo tofauti wakiwa na watu wengine waliratibu shughuli za kiharifu huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.


Katika shtaka la pili kati ya Januari Mosi ,2015 na Desemba 31,2017 katika eneo la Jangwani washtakiwa Robert,kulwa,Frorencia wakiwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil Gas Limited alijenga kituo cha mafuta kinachoitwa. Zenon Oil and Gas katika karakana ya Kampuni ya Udart bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma na Nishati na Maji(Ewura).


Shtaka la tatu kati ya Januari Mosi,2015 na Desemba 31,2017 katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam washtakiwa hao wakiwa wakurugenzi wa kampuni hiyo kwa pamoja walianzisha biashara ya kuuza mafuta ya petroli katika eneo ambalo halijaruhusiwa.


Katika shtaka la nne la utakatishaji, kati ya Mei 25, 2015 na Decembe 31, 2015 wakiwa jijini Dar es SAlaam washtakiwa hao waliibia Sh1,216,145,374 mali ya Kampuni ya UDART.


Shtaka la tano la utakatishaji wa fedha, inadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 katika jiji la Dar es Salaam Washtakiwa Robert, Kulwa, Charles na Frolencia wakiwa na lengo la kuficha uhalisia walibadilisha thamani ya mafuta kuwa fedha yenye thamani ya Sh 1, 216, 145, 374 kwa kuyauza wakati akijua mafuta hayo ni zao la uhalifu.


Pia shtaka la sita ni utakatishaji wa fedha washtakiwa hao wanadaiwa kuwa ambapo kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 wakiwa jijini Dar es Salaam waliweza kumiliki kiasi cha fedha hizo Sh1.216, 145, 374 huku wakijua ni zao la kosa la wizi.


Katika kosa la saba inadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 akiwa jijini Dar es Salaam kwa makusudi aliisababishia hasara UDART ya Sh.2.414, 326, 260.70.


Katika kosa la utakatishaji fedha linamkabili Robert Kisena na Chen Shi ambapo wanadaiwa Aprili 8, 2016 katika benki ya NMB Kisena akiwa Mkurugenzi wa UDART alihamisha Sh594.92 milioni kwenda kwenye akaunti nyingine ya Kampuni ya Longway Engineering Company wakati akijua fedha hizo ni zao haramu lililotokana na makosa ya kughushi.


Katika kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu linamkabili Kisena na Shi ambapo wanadaiwa walilitenda June 9, 2016 katika tawi la NMB Ilala ambapo kwa nia hovu waijipatia 603.25 milioni kutoka UDART kwa kuonyesha kiwango hicho kimelipwa kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Kituo cha UDART Kimara, Ferry (Kivukoni), Ubungo na Morocco  

Updated: 28.05.2019 14:06
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.