Kisena, wenzake waendelea kusota rumande

Kisena, wenzake waendelea kusota rumande

15 July 2019 Monday 15:16
Kisena, wenzake waendelea kusota rumande

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka, maarufu  Mwendokasi (UDART), Robert Kisena na wenzake, wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokukamilika.

Kisena na wenzake wanne, wakabiliwa na mashtaka 19, likiwemo la utakatishaji fedha na kuisababishia UDART hasara ya bilioni 2.

Wakili wa  Serikali, Wankyo Simon  ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Julai 15, 2019  kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Simon  ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina, wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

" Upelelezi wa kesi hii bado haujakamilika na siwezi kusema Upelelezi upo katika hatua gani, hivyo naiomba  mahakaka ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa"   alidia Simon

Hakimu Mhina, baada ya kusikiliza maelezo hayo, aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 30, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.

Mbali na Kisena , washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2019 ni mke wa Kisena, Florence Mashauri; Kulwa Kisena; raia wa China Chen Shi na Mhasibu wa Kampuni hiyo, Charles Selemani Newe.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kati ya Januari Mosi, 2011 na Mei 31,2018 ndani ya jiji la Dar es Salaam, waliongoza genge la uharifu.

Katika shtaka la pili, linawakabili washitakiwa wanne ambao ni Kisena, Kulwa, Simon na Florence ambalo ni kujenga kituo cha mafuta ya petroli bila kibali kutoka  EWURA.

Wanadaiwa kutenda  kosa hilo Januari Mosi mwaka 2015 na Desemba 31, 2017 ambapo inadaiwa walijenga kituo hicho eneo la Jangwani bila kibali cha EWURA.

Katika shtaka la tatu washitakiwa hao inadaiwa kwa kipindi hicho wakiwa wakurugenzi walifanya biashara eneo ambalo halijaruhusiwa kujengwa.

Pia katika shitaka la nne inadaiwa waliiba  bilioni 1.2  mali ya UDART huku mashtaka manne ni utakatishaji wa fedha.

Mengine ni mashtaka manne ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo; manne ya wizi; moja kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja ni kusababisha hasara UDART.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.