Kisena, wenzake waendelea kusota rumande

Kisena, wenzake waendelea kusota rumande

11 June 2019 Tuesday 16:47
Kisena, wenzake waendelea kusota rumande

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

Upelelezi wa kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka, maarufu kama Mwendokasi (Udart), Robert Kisena na wenzake , bado haujakamilika.

Hayo yameelezwa leo, Juni 11,2019 na wakili wa Serikali, Ester Martin, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile, wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Rwizile baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 24, 2019 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.

Mbali na Kisena, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2019 ni mke wa Kisena, Florence Mashauri; Kulwa Kisena; raia wa china Chen Shi na Mhasibu wa Kampuni hiyo, Charles Selemani.

Washtakiwa  pamoja  wakabiliwa na mashtaka 19, yakiwemo ya utakatishaji fedha na kuisababishia UDART hasara ya bilioni 2.

Updated: 11.06.2019 16:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.