banner68
banner58

LHRC yapinga hukumu ya kifo mahakamani

LHRC yapinga hukumu ya kifo mahakamani

10 October 2018 Wednesday 21:38
LHRC yapinga hukumu ya kifo mahakamani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimefungua kesi ya Kikatiba namba 22 ya mwaka 2018 kupinga uwepo wa adhabu ya lazima ya kifo (mandatory death penalty).

Hatua hiyo imetangazwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Felista Mauya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya 16 ya siku ya kupinga adhabu ya kifo Duniani.

“Oktoba 9, 2018 kama sehemu ya maadhimisho kituo kimefungua kesi hii ya kikatiba kwa kuzingatia mifano ya nchi jirani kama Kenya, Uganda na Malawi ambapo adhabu ya lazima ya kifo imefutwa kabisa,” amesema Mauya.

“Malawi ilifuta adhabu ya lazima ya kifo mwaka 2007 kupitia kesi ya Francis Kafantayeni dhidi ya Mwanasheria Mkuu ya (2007) MWHC 1, Uganda kupitia kesi ya Susan Kigula na wengine 416 dhidi ya Mwanasheria Mkuu, 2019 na hivi karibuni Kenya kwa kesi ya Francis Karioko Muruatetu na Wilson Thirimbu Mwangi dhidi ya Jamhuri, Madai Namba 16 ya 2015,” amefafanua.

Amesema hali hiyo inaifanya Tanzania kuwa nchi pekee yenye adhabu ya lazima ya kifo Afrika Mashariki.

Mauya amesema pamoja na jitihada za muda mrefu za kutaka adhabu ya kifo ifutwe lakini Tanzania bado adhabu ya kifo inatolewa kwa makosa mawili ikiwemo, mauaji chini ya kifungu cha 197 na Uhaini chini ya kifungu cha 39 (3) © kwenye kanuni za adhabu No. 16 ya 2002.

Amesema changamoto nyingine Tanzania bado haijaridhia “Mkataba wa pili wa nyongeza wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1989” unaotaka kufutwa kabisa kwa hukumu ya kifo kama ilivyopendekezwa kwenye mpango wa kujitathimini wa nchi wanachama wa umoja wa mataifa (Universal Periodic Review UPR) mwaka 2016 katika kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu kwa nchi wanachama wa umoja wa Mataifa.

Amesema kwa mujibu wa taarifa ya haki za binadamu ya mwaka 2017, takwimu zilizonukuliwa kuhusu hukumu ya kifo Tanzania zinaonesha watu 472 wamehukumiwa adhabu ya kifo, kati yao 452 wanaume na 20 wanawake. Katika orodha hiyo 228 wanasubiri hukumu zao kutekelezwa na 244 rufaa zao bado zinasikilizwa mbele ya Mahakama ya rufaa.

Aidha Tanzania kwa sasa iko katika hatua isiyo rasmi ya kupinga na kutotekeleza adhabu ya kifo (defector Moratorium) ingawa hakuna jitihada za lazima zilizochukuliwa kuonesha nia ya kuifanya hali hiyo kutambulika katika sheria na katika sera na hatimaye kufuta kabisa adhabu hiyo katika mfumo wa sheria.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.