Lissu, Spika Ndugai waanza kuchuana Mahakamani

Lissu, Spika Ndugai waanza kuchuana Mahakamani

14 August 2019 Wednesday 04:35
Lissu, Spika Ndugai waanza kuchuana Mahakamani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

KESI iliyofunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu,kupinga hatua ya Spika wa Bunge Job Ndugai kumvua ubunge, itaanza kusikilizwa Alhamisi, Agosti 15, mwaka huu.

Kesi hiyo namba 18 ya mwaka 2019, yaliyofunguliwa na Lissu kupitia kwa mawakili wake, itasikilizwa mbele ya Jaji Sirillius  Matupa wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dar es Salaam, kuanzia saa 3 asubuhi.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam iliyotolewa Jumanne, Agosti 13, 2019, mlalamikiwa ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anatakiwa kufika mahakamani hapo bila kukosa akiwa na nyaraka zote anazotakiwa kuwa nazo kwenye shauri hilo.

Kufuatia hali hiyo mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene ametoa wito kwa viongozi, wanachama, wafuasi wa chama hicho na Watanzania wote wanaopenda haki, demokrasia na utawala bora unaoheshimu sheria, mahali popote walipo kufuatilia kwa karibu mwenendo wa shauri hilo kuanzia hatua ya sasa.

“Huu ni muda wa kufika mahakamani kuungana pamoja na kusikiliza mapambano hayo ya kuitafuta haki ya Lissu mahakamani baada ya Spika Ndugai kutangaza kile alichodai ni kukoma ubunge wake mnamo Juni 29, mwaka huu, alipokuwa akiahirisha Bunge, Jijini Dodoma,’’ amesema Makene.

Juni 29, 2019 Spika Nduga alipokuwa akiahirisha kikao cha Bunge la Bajeti alitangaza kumvua ubunge Lissu ambaye alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashiriki.

Tayari aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu anasubiri kuapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CCM.

Hatua hiyo ni kufuatia kushinda bila kupingwa kutokana na kutokuwepo kwa mgombea yeyote wa vyama vya upinzani.

Updated: 14.08.2019 11:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.