banner68

Lugola amshusha Cheo Kamanda na Mkuu wa Kikosi

Lugola amshusha Cheo Kamanda na Mkuu wa Kikosi

06 July 2018 Friday 13:34
Lugola amshusha Cheo Kamanda na Mkuu wa Kikosi

Leo July 6, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema alitaka kuchukua uamuzi wa kumfukuza kazi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mbeya na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Kagera lakini Happy Birthday yake ndio imewaokoa.

Hata hivyo, Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwashusha vyeo Makamanda hao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lugola amesema wakati anaapishwa na Rais alimwambia anachukizwa na matukio ya ajali yanatotokea hasa ya Mbeya.

“Ajali nyingi zinatokea Mbeya ambapo ilinibidi niende kwa Kamati ya Usalama, nilibaini kitu kilichofanya nivunje Mabaraza ya Kamati ya Usalama barabarani,”.

Amesema kuwa alichobaini alitaka kujua kuna wajumbe wangapi lakini walishindwa kujua idadi, wala majina, pia wameshindwa kumpa taarifa ya kile wanachokifanya.

“Hivyo lazima nichukue hatua kali ili kunusuru maisha ya watu kwani Rais amechoka kutuma salamu za rambirambi,”.

Kutokana na hatua hiyo amesema anamuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, awashushe vyeo Makamanda hao kutokana na uzembe.

“Leo nilipanga niwafukuze watu kazi ila bahati nzuri kwao mimi nilizaliwa Ijumaa na kwa vile niliimbiwa wimbo wa Happy Birthday To You….nikaona nisiaribu furaha yangu, hivyo nikawaacha,”amesema.

Updated: 06.07.2018 13:42
Keywords:
KANGI LUGOLA
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.