Maajabu ya brigedia Hassan Ngwilizi!!!

"Aliongoza mapambano ya UKOMBOZI wakati wa operesheni ya kusitisha mapinduzi yaliyokuwa na lengo la kurejesha ukoloni katika nchi ya Sheli Sheli"

Maajabu ya brigedia Hassan Ngwilizi!!!

"Aliongoza mapambano ya UKOMBOZI wakati wa operesheni ya kusitisha mapinduzi yaliyokuwa na lengo la kurejesha ukoloni katika nchi ya Sheli Sheli"

20 May 2019 Monday 22:35
Maajabu ya brigedia Hassan Ngwilizi!!!

Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi amefariki  leo Mei 20, 2019 katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam alipokuwa akitibiwa.

HISTORIA YAKE

Kamanda Shupavu Uliyekuwa miongoni mwa Makamanda muhimu sana walioongoza mapambano, medani na lojistiki za Kijeshi katika Vita vya Uganda,

Kamanda Shupavu Uliyeongoza Mapambano ya UKOMBOZI wakati wa operesheni ya kusitisha mapinduzi yaliyokuwa na lengo la kurejesha ukoloni katika nchi ya Sheli Sheli na Ulipomaliza kuzima Mapinduzi ukaiongoza nchi hiyo kama Mkuu wa NCHI wakati wa Kipindi cha Mpito kwa miaka mitano;

Kamanda Shupavu Uliyeongoza mapambano yaliyomaliza uasi wa RENAMO nchini Msumbiji hadi pale RENAMO waliposalimu Amri na kukubali kujigeuza kuwa Chama cha Siasa badala ya Chama cha Msituni;

Kamanda Shupavu Uliyetoa mchango muhimu wa Kijeshi na Intelijensia ya Kijeshi katika mapambano ya Uhuru wa Zimbabwe;

Kamanda Shupavu uliyetoa mchango muhimu wa Kiintelijensia ya Kijeshi katika mapambano ya Uhuru wa Namibia, na pia kutoa mchango muhimu katika harakati za vyama vya  Ukombozi vya PLO, FRELIMO, ANC, MPLA, ZANU PF, ZAPU, SWAPO, na hata PAC;

Kamanda, hutaweza kusahauliwa na Makamanda wenzako kwa weledi Wako. Kamanda Museveni, Kamanda Kagame, Kamanda Kabila, Kamanda Garang, na wengine wengi SANA.

Utumishi wako ukiwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam na hatimaye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hautosahaulika hasa tukio la kumwaga maelfu ya tani za ngano ambazo zilikuwa ziuzwe kwa wananchi licha ya kuwa hazikuwa fit for human consumption. Utakumbukwa na wengi hasa sisi wanafunzi wako wa uraia, uongozi na hata uliowafundisha kwenye mafunzo ya Kijeshi. watakukumbuka DAIMA. Tusalimie akina Mzee Nnauye na Akina Mzee Laurence Gama.

Utumishi wako katika Chama hasa ulipokuwa NKM CCM uliwagusa wengi. Pia ulipokuwa Mbunge na Waziri. Miongoni mwa mambo ya kukumbukwa ni barua yako uliyowaandikia Mawaziri wa Wizara nyingine waliokuwa wanaatamia fedha katika Makao Makuu ya Wizara zao badala ya kuzipeleka fedha hizo kwenye Serikali za mitaa ambako zingetekeleza miradi ya wananchi moja kwa moja.

Utakumbukwa kwa agizo la O&OD serikalini na mengine meengi. Hakika ulikuwa taa. Miongoni mwa taa zetu imezimika. Nilipokutana na wewe mara ya mwisho mwezi Novemba 2017 uliniambia "nakukumbuka vizuri kijana, tumia ujasiri uleule. Piga KAZI local government ni ngumu inahitaji sana ujasiri" wakati huo nilikuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.        Mzee;! Nitakukumbuka Daima. Ni Mimi Joseph George J.C.J.N.N.K.K.M.M. Kakunda.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.