Madereva bajaji Mbeya wawekwa 'mtegoni'

Madereva bajaji Mbeya wawekwa 'mtegoni'

15 July 2019 Monday 13:45
Madereva bajaji Mbeya wawekwa 'mtegoni'

Na mwandishi wetu,  Mbeya. 
 MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imesema itawakamata na kuwatoza faini madereva bajaji wanaobeba abiria kutoka kwenye vituo vya  daladala. Vile vile  wanatakiwa wafuate sheria na kanuni n za usafirishaji zilizopo.

Meneja wa Latra Kanda hiyo, Denis Daudi amesema hatua hiyo inatoka na madereva bajaji kukiuka masharti(kanuni) za leseni za matumizi ya vyombo hivyo.

 "Kwa mujibu wa sheria, usafiri wa bajaji unapaswa kukodiwa na si kuchukua abiria katika vituo vya daladala, kufanya hivyo ni makosa kisheria, tutawasaka na kuwatoza faini na hata kuwachukulia hatua nyingine za kisheria'' amesema Daudi na kuongeza

"Mwezi Machi mwaka huu kulitokea mgomo wa daladala na sababu kubwa ilikuwa ni bajaji   jambo lililotulazimu  kukaa kikao na   kutoa maelekezo ambayo yalileta mafanikio   cha kushangaza wanarudia tena"

Mwenyekiti wa waendesha bajaji Jiji la Mbeya, Idd Ramadhani amesema kutokana na  changamoto hiyo wamelazimika kukaa kwenye vituo vya daladala kufanya operesheni ya kuwakamata madereva wanaokiuka sheria za usafirishaji.

"Kimsingi  bajaji inapaswa kukodiwa na si kuchukua abiria  kama daladala na ndio maana kulitokea mgomo  na chanzo kilikuwa ni bajaji sasa tumejiwekea mikakati kwa atakayebainika akichukua abiri tunamkamata na   faini 10,000"amesema

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.