Madereva, makodakta wa daladala wenye lugha chafu kukamatwa

Madereva, makodakta wa daladala wenye lugha chafu kukamatwa

20 September 2019 Friday 10:04
Madereva, makodakta wa daladala wenye lugha chafu kukamatwa

Na mwandishi wetu, Mbeya.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, (LATRA) imesema inawachunguza na itawachukuli hatua za kisheria Madereva na Makondakta watakaobainika kutumia lugha chafu kwa abiria.

Meneja wa LATRA Kanda hiyo, Denis Daudi amesema hatua hiyo inafuatia baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa abiria wanaodai tiketi wanaposafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani na nje ya jiji la Mbeya.

‘‘Kodakta au dereva hapaswi kukiuka sheria na taratibu zilizoweka ikiwamo kutoa lugha chafu kwa abiria. Naomba abiria wanapopata shida hii, walete malalamiko yao katika ofisi yetu na hata kwa askari wa barabarani (Trafiki),’’ amesema na kuongeza

‘‘Sheria ipo na kwa mujibu wa sheria adhabu atakazokutana nazo dereva au kodakta ni kutozwa faini ya Sh 50,000 au kufikishwa mahakamani.’’

Abiria wanaosafiri kutoka Stend Kuu ya Mabasi ya Mikoani kuelekea katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbalizi , na kutoka Sokomatola kwenda Uyole wamelalamikia kuwepo kwa baadhi ya makondakta kutokuwa wastaarabu na kutumia lugha za kejeli pindi wanapodaiwa tiketi.

Tumpale Saimon amesema ipo haja ya vyombo husika kufanya uchunguzi na kuwawajibisha ili waweze kutambua majukumu yao na kutii sheria bila shuluti .

Gwamaka Fredy Mkazi wa Iyunga ameishauri Serikali kufanya usajili wa makondakta na Madereva pamoja na wamiliki wa makampuni waliyowaajiri ili yanapojitokeza majanga hususan ya ajali, ukikwaji wa sheria iwe rahisi kuwabaini na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.