Mafunzo matumizi uandikishaji wapiga kura kwa BVR yaiva

Mafunzo matumizi uandikishaji wapiga kura kwa BVR yaiva

16 July 2019 Tuesday 10:55
Mafunzo matumizi uandikishaji wapiga kura kwa BVR yaiva

Na mwandishi wetu, Hai
WAANDISHI wasaidizi wa BVR Kit Operators kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wakiendelea na mafunzo juu ya matumizi ya BVR kwa ajili ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajiwa kuzinduliwa Julai 18, 2019 mkoani humo.

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa atazindua zoezi hilo litakalofanyika nchini kote katika hafla itakayofanyika katika viwanja vya Mandela eneo la Pasua Kata ya Bomambuzi, Manispaa ya Moshi.

Tume ya taifa ya Uchaguzi(NEC) imewataka wakazi wa Manispaa  hiyo na maeneo mengine ya Mkoa wa Kilimanjaro  kushiriki katika sherehe  hizo.

Baadhi ya waandishi wasaidizi wa BVR Kit Operators wakiendelea na mafunzo ya matumizi ya vifaa hivyo kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.