banner68
banner58

Magufuli aagiza Chama cha Wanasheria Tanganyika kudhibitiwa

Alitoa agizo hilo muda mfupi leo jijini Dar es Salaam mara baaada ya kuwaapisha Majaji kumi wa mahakamu kuu

Magufuli aagiza Chama cha Wanasheria Tanganyika kudhibitiwa

Alitoa agizo hilo muda mfupi leo jijini Dar es Salaam mara baaada ya kuwaapisha Majaji kumi wa mahakamu kuu

20 April 2018 Friday 13:22
Magufuli aagiza Chama cha Wanasheria Tanganyika kudhibitiwa

Na Mwandishi Wetu

RAIS John Magufuli amewataka majaji nchini kuhakikisha kuwa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) kinakuwa mali ya umma na si binafsi.

Alitoa agizo hilo muda mfupi leo jijini Dar es Salaam mara baaada ya kuwaapisha Majaji kumi wa mahakamu kuu ambao waliteuliwa wiki iliyopita.

Alisema kuwa TLS isikose kudhibitiwa kwani serikali inataka kiwe na nidhamu na kuahidi kuisimamia.

“Mali yenu isiwe ya binafsi, TLS isikose control (kudhibitiwa) tunataka nidhamu, tutasimamia nidhamu,” alisema mkuu huyo wa nchi.

Aidha Rais Magufuli aliwataka Majaji aliowateua kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kila jambo watakalo kuwa wanalifanya kwa maslahi ya Taifa.

“Kazi ya Ujaji ni ngumu sana mtangulizeni Mungu, mathalani sasa tuko katika vita ya uchumi ambayo ni kama kuomba uhuru,” aliongeza.

Alimshukuru Waziri wa Katiba na Sheria Prof Palamagamba Kabudi, vyombo vya ulinzi na usalama kwa kumsaidia kuteua majaji hao.

Aliahidi kushughulikia maslahi ya majaji hao na kuwataka kufanya kazi kwa kutozingatia maoni ya mitandao ya kijamiii ambayo imekuwa ikipotosha umma kwa malengo yao binafsi.

Alisema kuwa si kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni kweli, na kuwataka majaji hao kuwachukulia hatua watu wanaojihusisha na kutuma taarifa zisizo rasmi.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, aliwataka majaji nchini kuharakisha usikilizaji wa kesi na kutoa uamuzi haraka.

Alisisitiza usikilizaji wa kesi hasa zile zinazohusu kodi na kuwaomba kuziondoa haraka mezani mwao ili wasije kufuatwa fuatwa.

Azania Post

Updated: 20.04.2018 14:46
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.