Magufuli aendesha gari la JWTZ kwa 'mbwembwe'

Magufuli aendesha gari la JWTZ kwa 'mbwembwe'

12 September 2019 Thursday 19:34
Magufuli aendesha gari la JWTZ kwa 'mbwembwe'

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping kwa kuuendeleza ushirikiano na uhusiano mzuri wa Tanzania na China ikiwemo misaada na uwekezaji ambao China inaufanya hapa nchini.

Magufuli ametoa shukrani hizo leo Septemba 12, 2019 jijini Dar es Salaam katika hafla ya makabidhiano ya magari 40 kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) kwenda Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyofanyika katika Makao Makuu ya JWTZ Upanga Jijini DSM.

Mara baada ya kukabidhiwa rais Magufuli aliendesha moja ya gari hilo kwa mbwembwe huku akiwa amempandisha mkuu wa majeshi, Venas Mabeyo

PICHANI JUU : Rais Magufuli akiendesha moja ya magari 40 yaliyokabidhiwa kwa jeshi la Tanzania(JWTZ)kutoka kwa jeshi la ukombozi la watu wa China(PLA)

Updated: 12.09.2019 19:40
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.