banner58

Magufuli aionyeshea kidole Benki ya Maendeleo ya Wakulima, yakalia kuti kavu

Alisema kuwa haoni sababu inayokwamisha kutumia fursa mbali mbali za kilimo kwa ajili ya maendeleo

Magufuli aionyeshea kidole Benki ya Maendeleo ya Wakulima, yakalia kuti kavu

Alisema kuwa haoni sababu inayokwamisha kutumia fursa mbali mbali za kilimo kwa ajili ya maendeleo

04 June 2018 Monday 12:25
Magufuli aionyeshea kidole Benki ya Maendeleo ya Wakulima, yakalia kuti kavu

Na Mwandishi Wetu

RAIS Dk John Magufuli amesema hajaridhika na utendaji wa benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) na wala hajui kama Mkurugenzi Mtendaji wake bado yupo kazini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDPII), leo jijini Dar es Salaam, Magufuli alisema kuwa wakulima bado hawajanufaika na uwepo wa benki hiyo kwani mtaji iliyopata imekuwa ikiwakopesha wafanyabiashara wakubwa na kufanya biashara na benki nyingine.

Akitolea mfano alisema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Disemba mwaka jana benki hiyo ilikopesha mabenki mengine kiasi cha shilingi bilioni 82.3 huku wakulima wakitengewa shilingi bilioni 5.9 tu.

“Bado sijaridhika na utendaji wa benki hii, iliyoanzishwa mwaka 2014 kwa mtaji wa shilingi bilioni 60,” alisema Magufuli.

Aliongeza kuwa hafahamu kama mkurugenzi wa benki hiyo bado anafanya kazi na kushauri kuwa ingeweza kutoa mikopo kwa kupitia dhamana ya wakuu wa mikoa.

Aliiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhakikisha TADB inabadilika na kuhakikisha kuwa wakulima wanakopesha na akaahidi kufuatilia yeye mwenyewe kama jambo hilo litafanyika.

Akielezea zaidi, Dk Magufuli alisema kuwa Tanzania ina hekta milioni 44 lakini ni hekta milioni mbili zinafaa kwa umwagiliaji na kuwataka wanaohusika kuhakikisha kuwa jambo hilo linafanyika kweli.

Alisema kuwa haoni sababu inayokwamisha kutumia fursa mbali mbali za kilimo kwa ajili ya maendeleo.

Alitaja sababu zinazokwamisha kilimo kuwa ni mbinu duni za kilimo, kukosekana kwa huduma za kifedha, ukosefu wa masoko na ukosefu wa usafiri, umeme na maghala ya kuhifadhia mazao na kuwataka wadau kushirikiana kuziondoa.

Alisema kuwa ASDPII inatakiwa kuweka kipaumbele uzalishaji wa mazao ya kilimo, mbolea na viutatilifu na mazao ya kimkakati.

Alidokeza kuwa mwaka jana Tanzania ilipata hasa ya zaidi ya shilingi billion 64 zilizotokana na pembejeo hewa na kuwataka viongozi kujiepusha na hilo katika programu hii.

Aliwahakikishia wafadhili kuwa fedha yao itatumika kwa jinsi iliyopangwa na kuwataka watendaji wa serikali kusimamia hilo.

Aidha aliwataka maafisa ugani wa kilimo kuacha kukaa ofisini, na badala yake waende mashambani kwa ajili ya kuwasaidia wakulima

Awali Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba alisema kuwa zaidi ya shilingi trilioni 13 zinatarajiwa kutumika katika awamu ya pili ya program hiyo kwa kipindi cha miaka mitano. Alisema kuwa kwa mwaka wa kwanza serikali imeahidi kutoa shilingi bilioni 943 ambapo nchi wafadhili watatoa shilingi trilioni 1.9.

Alibainisha kuwa kilimo cha mazao mkakati kitaongezeka huku akitolea Pamba kuwa itafikia tani laki sita mwaka huu kulinganisha na tani 133,000 mwaka jana.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.