Magufuli ajutia kuwa rais

Magufuli ajutia kuwa rais

04 October 2019 Friday 17:21
Magufuli ajutia kuwa rais


Mwandishi wetu, Songwe
RAIS John Magufuli amesema anajutia kwa kihelehela chake cha kujazafomu ya kugombea nafasi hiyo na  amewaomba viongozi wa dini kumwombea kutoka na ugumu wa kazi alionayo 

Magufuli amesema hayo leo Oktoba 4, 2019 wakati akiongea na wananchi wa mji Wa Mlowo mkoani Songwe kwenye ziara yake ya  kikazi mkoani humo.

"Ndugu zangu kazi hii ni ngumu sana hata mawaziri wangu hawalali usingizi na hawajui kama kesho yake wataamka wakiwa katika nafasi zao," amesema.

Amesema kila unapoangalia kusonga mbele ujue kuna maadui sasa lazima tuchape kazi kwa kumtanguliza Mungu na wale waliojitoa ufahamu Mungu awasaidie.

"Eti  mtu wa  chama fulani anafurahia.  ndege ya Tanzania kushikiliwa katika nchi nyingine, ninawaomba viongozi  wa dini kubeba jukumu la kuliombea hilo," amesema Magufuli.

Pamoja na mambo mengine amesema serikali imetoa billion 18 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Songwe (SIA)  na mkandarasi anaendelea na kazi, lengo likiwa ni kwa ndege kubwa kutua.
 

Vilevile rais Magufuli  ameimiza upendo ,amani, ushirikiano kwa watanzania wote na kumtangyuliza Mungu kwa kila jambo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.