Magufuli amfuta kazi Junuary Makamba, Bashe akumbukwa

Magufuli amfuta kazi Junuary Makamba, Bashe akumbukwa

21 July 2019 Sunday 07:43
Magufuli amfuta kazi Junuary Makamba, Bashe akumbukwa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS John Magufuli amemteua George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Anachukua nafasi ya January Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Taarifa ya Ikulu leo Julai 21, 2019 inaeleza kuwa rais Magufuli pia amemteua Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Bashe anachukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa Biashara na Uwekezaji.

Katika hatua nyingine, rais Magufuli amemteua Balozi Dk. Martin Lumbanga kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa manunuzi wa umma(PPRA)

Balozi Lumbanga ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili. Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo Julai 21, 2019

Kupitia akaunti yake ya Twitta, mapema leo January amesema'' Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko kwa moyo  mweupe kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo''

Updated: 21.07.2019 08:11
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.