Magufuli amjulia hali Maria Nyerere, atoka hospitali

Magufuli amjulia hali Maria Nyerere, atoka hospitali

10 June 2019 Monday 19:52
Magufuli amjulia hali Maria Nyerere, atoka hospitali

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

HALI ya afya ya mke wa zamani wa rais wa Tanzania, Maria Nyerere imezidi kuimarika na ameruhusiwa kurudi nyumbani.

Hii leo Juni 10, 2019 rais John Magufuli na mkewe Janeth Magufuli wamemjulia hali nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine wamemuombea dua.

 Juni 6, 2019 Maria Nyerere alirejeshwa kwa ndege maalumu kutoka nchini Uganda alikokuwa katika ibada ya sherehe  za siku ya mashahidi  ambako afya yake ilizorota.

 Juni 8,2019 Mke wa rais Magufulu, Janeth Magufuli alimtembelea  hospitalini jijini Dar es Salaam.

Rais wa Uganda ,Yoweri Museveni  ndiye aliyetoa ndege rasmi ya kumrejesha nyumbani Maria Nyerere ambaye kila mwaka hudhuru nchini Uganda kwa ajili ya ibada hiyo inayofanyika Namugongo

Rais Museveni ariripotiwa kutohudhuria sherehe za siku ya mashahidi wa Uganda katika eneo la Namugongo kwa ajili ya kumtembelea Mama Maria mjini Kampala katika  moja ya hospitali mjini humo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.