Magufuli amteua Julius Mtatiro kuwa mkuu wa wilaya

Magufuli amteua Julius Mtatiro kuwa mkuu wa wilaya

14 July 2019 Sunday 08:07
Magufuli amteua Julius Mtatiro kuwa mkuu wa wilaya

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
RAIS John Magufuli amemteua Julius Mtatiro kuwa mkuu wa wilay ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Taarifa ya mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, ya leo Julai 14, 2019 inaeleza kuwa Mtatiro anachukua nafasi ya Juma Zuberi Homera ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi.

''Uteuzi huo wa Mtatiro umeanza leo Julai 14, 2019,'' inaeleza taarifa hiyo

Julai 11,2018 Mtatiro aliibua maswali mengi mara baada kujivua uanachama wa chama cha wananchi (CUF) na kujiunga  na chama tawala CCM

Mtatiro ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa  kamati ya uongozi ya CUF ambaye pia ni mchambuzi wa siasa na alikuwa akiandika makala nyingi kuikosoa serikali.

"Nimejiridhisha kwa hitaji la nafsi yangu kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM" Julius Mtatiro aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumamosi Agosti 11, 2018

Hata hivyo mkurugenziwa habari wa chama cha CUF, Abdul Kambaya alisema zaidi ya asilimia 70 ya migogoro ya chama hicho ilisababishwa na Mtatiro

Updated: 14.07.2019 08:55
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.