Magufuli ashtukia dili wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi

Magufuli ashtukia dili wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi

16 July 2019 Tuesday 06:27
Magufuli ashtukia dili wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi

YALIYOJIRI  JULAI 15, 2019 WAKATI WA UZINDUZI WA HUDUMA TIBA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO, JIJINI MWANZA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema:

#Kupeleka wagonjwa nje ilikua ni dili na ni fursa kwa watu wengine  na bili zote zilikua zinalipwa na Serikali ya Tanzania hivyo namuagiza Waziri wa afya afuatilie malipo yote yanayotakiwa kulipwa nje kwani mengine sio ya haki.

#Lazima Waziri wa Afya uanze kufuatilia vizuri na kwa umakini wagonjwa wanaotakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, tusiwafanye watu kwenda nje kufanya utalii kwa gharama za matibabu.

#Natoa rai kwa Hospitali ya Bugando kuendeleza utengenezaji wa oxygen  na maji ya dripu kwa wingi zaidi ili tuache kuagiza nje, tununue hapa hapa ili kutengeneza ajira na kupunguza gharama za manunuzi.

#Kama mnataka mkopo wa kujenga kiwanda kikubwa hapa Bugando kutoka kwenye mabenki mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha utengenezaji wa vitu hivyo niko tayari kuwasaidia.

#Hospitali hii ni ya mfano kwani haina ubaguzi, mfano huu sisi Watanzania tunatakiwa kuuenzi, ni ya wakatoliki lakini wanahudumia wagonjwa wa dini zote.

#Nasema kwa dhati Serikali itaendelea kushirikiana na hospitali zinazoendeshwa na madhehebu ya kidini ili kuhakikisha afya za watanzania zinaboreshwa, pia naomba mtuvumilie pale tunapoingilia kati kuchunguza juu ya huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hizo.

#Nawapongeza kwa kuwahudumia hata wasio na pesa pia kwa kuanzisha kitengo cha Bima ya afya ili watanzania hata wa hali ya chini waweze kutibiwa hapa.

#Tumetenga shilingi Bil.152 kwa ajili ya kujenga meli na tunakarabati meli zingne tano ili wananchi wa Kanda ya Ziwa wafanye biashara kwa ajili ya maendeleo yao.

#Tumetenga takriban Bil.700 kwa ajili ya kujenga daraja refu litakalopita majini na kandarasi ameshapatikana hivyo naagiza ndani ya wiki moja Wizara ya Ujenzi na TANROADS wawe wameshasaini mkataba wa kujenga daraja hilo ili ndani ya miezi miwili ujenzi uanze.

#Naagiza wataalam wa Wizara ya Afya mkatafute chanjo na kufanya utafiti kufahamu kwanini asilimia kubwa ya wagonjwa wa saratani na magonjwa ya moyo wanatoka sana Kanda ya Ziwa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Mhe. Ummy Mwalimu

#Tunakuhakikishia kuwa Wizara ya Afya tutaendelea kutekekeza Sera ya Taifa ya Afya ya Mwaka 2007 na maelekezo ya Ilani ya CCM ya uwekezaji katika Sekta ya Afya.

#Hadi kufikia Juni 30 2019, tunavyo vituo vya kutolea huduma za afya 8119.

#Tutaendelea kuweka mikakati kwa kushirikiana na taasisi za dini ili kuhakikisha tunapeleka huduma bora za wananchi kote nchini.

#Mhe Rais Magufuli uamuzi wako wa kuongeza bajeti ya dawa umewezesha kuongeza bajeti ya dawa za Saratani kutoka Tsh Milioni 700 hadi Tsh Bil.10.

#Katika Bajeti ya Mwaka huu tumetenga Tsh Bil. 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa wodi za wagonjwa wa saratani katika hospitali hii.

#Kutokana na mabadiliko tuliyoyafanya katika hospitali hii ya usimamizi wa mapato na utoaji huduma, Mapato yameongezeka kutoka Tsh Bil. 1.2 kwa mwezi 2016 hadi kufikia Bil. 3.9 kwa mwezi, mwaka 2019.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Prof. Joyce Ndalichako

#Nikupongeze Mhe. Rais Magufuli kuwa mstari wa mbele kuhakikisha huduma za wananchi zimarishwa.

#Tume ya Nguvu za Atomiki, Wizara yangu pamoja na Wizara ya Afya tumewezesha kupatikana kwa mashine kwa ajili ya tiba ya saratani katika hospitali hii ya Bugando ambayo ni mkombozi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa.

#Tutaendelea kuhakikisha matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi inapelekwa katika maeneo mengi nchini ili kupunguza mzigo kwa wananchi kufuata huduma Dar es Salaam, sasa tunaanza na Nyanda za Juu Kusini.

Mwenyekiti  wa Bodi ya Udhamini wa Hospitali ya Bugando, Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Renatus Nkwande

#Utoaji wa Huduma za saratani ni kubwa hivyo kwa msaada wa serikali tunaamini huduma zitaendelea vizuri.

#Tunakupongeza Mhe Rais Magufuli kwa jitihada zako za kuboresha huduma za afya nchini.

#Huduma hii itasaidia sana kuondoa adha waliokuwa wanaipata wagonjwa kwenda hadi kufuata huduma hii Dar es Salaam.

IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO

Updated: 16.07.2019 06:45
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.