Magufuli: Ata mimi naweza kuwa mfungwa mtarajiwa!

Magufuli: Ata mimi naweza kuwa mfungwa mtarajiwa!

16 July 2019 Tuesday 14:30
Magufuli: Ata mimi naweza kuwa mfungwa mtarajiwa!

Na mwandishi wetu, Mwanza
RAIS John Magufuli amesema ata yeye anaweza kuwa  kama mfungwa mtarajiwa.

Amesema hayo leo Julai 16, 2019   katika ziara yake ya kushtukiza alipokuwa akizungumza na wafungwa na mahabusu katika Gezeza Kuu la Butimba jijini Mwanza na amewapa zawadi ya ng’ombe watatu na magunia 15 ya mchele.

Awali wafungwa na mahabusu hao walitoa kero zao kwa rais na kuwatuhumu baadhi ya  askari magereza wanawafanyia mambo yasiyostahili.

Mfungwa Kalikenya Nyamboge anayetumukia kifungo cha miaka 30  amemtuhumu Ofisa Usalama gerezani hapo kuwapa wafungwa simu halafu zikikamatwa wananyan’ganywa vitu vyao walivyo navyo lakini hadi leo hajafanywa kitu chochote.

“Mheshimiwa rais, huyu ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakuwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru.

“Sasa hivi Jenerali Kamishna ametuletea daktari msomi na alivyofika vifo ndiyo vimepungua maana walikua wakikuchoma sindano wanakuua.

“Na si mara ya kwanza wao kuua mimi nilikuwa nimepanga nikitoka nije kukwambia na nikitoka nitakuletea mambo yote yanayotokea huku lakini huyu usimuache maana kwa Mwenyezi Mungu utakua umeandika maelezo ya mauji,” amesema Nyamboge.

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mbugani, Hashimu Kijuu, amesema yeye yuko gerezani hapo kwa kupewa kesi ya utakatishaji baada ya kuuza shamba lake huku askari mmoja aliyemtaja kwa jina la Sangali akimwambia ataozea jela.

“Mimi niliuza shamba langu lililopo Kisesa jijini Mwanza lakini matokeo yake Sangali aliniambia nitakaa jela hadi nitakapokuta mke wangu ameolewa, sasa ni maneno gani hayo,” amesema Kijuu na kuongeza

"Mfungwa, Kulwa Alphonce, alikamatwa mwaka 2017 akiwa na mafuta ya dizeli akapelekwa Kituo cha Nyegezi askari wakamuomba Sh milioni moja, akawaambia ana 200,000 tu ambayo walikataa kisha baadaye wakampeleka ‘central’ baada ya hapo akafunguliwa kesi ya mauaji''

Mfungwa mwingine Shukrani Masegenya, alimuomba rais Magufuli kuwapunguzia adhabu ya vifungo ili wakatumie ujuzi wao wanaofundishwa nje.

Updated: 16.07.2019 14:50
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.