Magufuli awalilia wafanyakazi Azam Media

Magufuli awalilia wafanyakazi Azam Media

08 July 2019 Monday 14:08
Magufuli awalilia wafanyakazi Azam Media

Na mwandishi wetu

RAIS  John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa mwenyekiti wa kampuni  za  Said  Salim Bakhresa  kufuatia   vifo  vya  wafanyakazi  5  wa  vyombo  vya    habari  vya Azam Media Limited vilivyotokea leo  Julai 8, 2019 katika ajali barabarani.

Ajali hiyo  imetokea majira ya saa 2:30 asubuhi katika  eneo la Kizonzo katikati ya  Igunga(Taboro) na Shelui (Singida)  ambapo  basi  aina ya  Coaster lililowabeba  wafanyakazi  wa  Azam  Media  Limited  likielekea  Mwanza limegongana uso kwa na uso na Lori la  mizigo  lililokuwa   Iinakwenda   Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Azam TV waliofariki kwenye ajali hiyo ni Salim Mhando (muongozaji wa matangazo), Florence Ndibalema (Mhandisi wa Sauti), Sylvanus Kasongo (Mhandisi Mitambo) na wapiga picha wawili Said Haji na Charles Wandwi.

Watu wengine wawili waliofariki ni dereva wa gari ambalo Azam TV walilikodi pamoja na msaidizi wake, majina ya wawili hao bado hayajapatikana. Wafanyakazi watatu wa Azam TV waliojeruhiwa ni Artus Masawe, Mohammed Mwinshehe na Mohammed Mainde.

Wafanyakazi wa Azam Media limited walikuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa hifadhi va Taifa va Burigi-Chato kwa ajili va kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hizo.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na taarifa za ajali iliyosababisha vifo vya watu 7 wakiwemo wafanyakazi  hao 5, dereva na msaidizi wake. Amewaombea marehemu wote wapumzike mahala pema peponi 

"Nimeshtushwa sana na vifo hivi, nampa pole Mwenyektti Ndg. Said Salim Bokharesa Na, nduga wa Marehernu wote, Mtendail Mkuu Ndg. Tido Mhondo na wafanyakazi  wote wa Azam  Media Ltd, waandishi wa habari wote na watu wote waliaguswa na vifo hivi,'' amesema rais Magufuli

Rais Magufuli amewaombea majeruhi 3 wa  ajali  hiyo wapone  haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Aidha, rais Magufuli  amerejea  wito wake  wa kuwataka watumiaji wa barabara  hususani madereva   kuwa makini   na  kuzingatia   sheria  za  usalama barabara ili kuepusha ajali  zinazoweza  kuepukika.

PICHANI JUU; Ndio  magari yaliyogongana

PICHA CHINI; Wafanyakazi wa Azam Media waliofariki  katika ajali hiyo

Updated: 09.07.2019 06:29
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.