banner68
banner58

Magufuli, Kikwete awaongoza mamia kuaga Mzee Majuto

Magufuli, Kikwete awaongoza mamia kuaga Mzee Majuto

09 August 2018 Thursday 15:06
Magufuli, Kikwete awaongoza mamia kuaga Mzee Majuto

Rais wa Tanzania, John Magufuli na Rais mstaafu Jakaya Kikwete amewaongoza mamia ya Watanzania kuaga mwili wa marehemu muigizaji wa vichekesho Amri Athumani 'Mzee Majuto” kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

Mwili wa Mzee Majuto uliwasili Ukumbini hapo saa nane na shughuli ya kuaga ikaanza ikiwemo salamu za rambirambi na dua ya kuombea iliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na vya kijamii na viongozi wa dini wameungana na waigizaji wenzake na marehemu pamoja na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Mzee Majuto aliaga dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya taifa Muhimbili jijini dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Updated: 09.08.2018 15:09
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
desmo berry 2018-08-09 16:28:31

r.i.p mzee majuto

Avatar
baraka boyka 2018-08-09 20:15:52

rip mshefaa mungu akulaze mahali pema peponi

Avatar
MUHIDINI AWADHI 2018-09-03 12:27:46

MUNGU AMJAZIE NURU NA ALALE MAALI PEMA AMI