Magufuli kuungana na Waislam mchana Mnazi Mmoja, Polisi watoa kauli

Magufuli kuungana na Waislam mchana Mnazi Mmoja, Polisi watoa kauli

15 June 2018 Friday 10:36
Magufuli kuungana na Waislam mchana Mnazi Mmoja, Polisi watoa kauli

Na Mwandishi Wetu

RAIS Dk John Magufuli mchana wa leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Idd litakalofanyika kwenye viwanja ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salum, Baraza hilo litafanyika kuanzia saa tisa alasiri.

Aliwataka Waislam wote kuhudhuria kwa wingi kwenye baraza hilo kwa ajili ya kusikiliza ujumbe utakaotolewa na kiongozi huyo wa kitaifa.

Waislam nchini leo wameungana na wenzao duniani kwa kusherehea sikukuu ya Eid El Fiftri mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhan na kuonekana kwa mwezi jana usiku.

Tayari Polisi jijini Dar es Salaam imetoa kauli na kuwataka wananchi kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu huku ikiimarisha ulinzi maeneo mbali mbali.

Jeshi hilo pia limewataka wananchi kutokunywa pombe kwa zaidi na kuchukua tahadhari wawapo matembezini.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.