Magufuli:Wivu ndio sababu kukamatwa ndege ya Tanzania

Magufuli:Wivu ndio sababu kukamatwa ndege ya Tanzania

16 September 2019 Monday 17:02
Magufuli:Wivu ndio sababu kukamatwa ndege ya Tanzania

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

RAIS John Magufuli amesema wivu binafsi ndio sababu ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kumatwa nchini Afrika Kusini na hiyo ni kutokana na shirika hilo kuanza kuimarika na kuteka masoko mbalimbli ndani na nje ya Afrika.

Amesema hayo leo Septemba 16, 2019 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua kituo cha mfumo wa rada ya kuongozea ndege katika kituo cha Dar es Salaam, ambayo ni moja ya rada mpya nne zitakazofungwa nchini na kuwezesha kuona na kuongoza ndege katika anga lote la Tanzania.

“Ukiona hadi watu wanakamata ndege zetu basi ujue shirika letu linafanya kazi vizuri,” amesema Magufuli

Amesema licha ya kukamatwa kwa ndege hiyo (ambayo tayari imeshaachiliwa) itaendelea kuchapaka kazi, huku akitolea mfano kutoka kwenye mashairi ya wimbo wa kundi la Sauti Sol la Kenya, wimbo unaoitwa Extravaganza ambao mashairi hayo yanasema, wakifunika, tunafunua, wakianika, tunaanua, wakitufungia milango, wanatukuta ndani.

Rais ametoa pongezi kwa ATCL kwa namna linavyoimarika na kwamba hadi sasa linamiliki asilimia 75 ya sokola safari za ndani.

‘‘Tayari shirika hili limeanza safari za kimataifa, na karibuni litaanza kwenda China, hivyo ni lazima washindani wake waone wivu’’ amesema.

Kuhusu rada iliyopaswa kununuliwa kipindi cha nyuma, rais ameonesha kukerwa kwamba fedha za Watanzania zilitafunwa na watu wachache na rada hiyo iliyokuwa inunuliwe nchini Uingereza haikusimikwa tena, hivyo mabilioni ya fedha yakawa yamepotea.

Amesema aliwashangaa waliohusika kwenye sakata hilo kutokujiuzulu, huku wale wa upande wa Uingereza walijiuzulu.

Baada ya mifumo mipya ya rada za kuongozea ndege kukamilika kusimikwa, Tanzania itaweza kuona na kuongoza angala lote la nchi, tofauti na awali ambapo ilikuwa inaweza kuongoza asilimia 25 pekee ya anga lote.

Kuwa na uwezo wa kuongoza anga lote kutaongeza mapato ya serikali, kutaongeza kasi ya ndege kuweza kuruka na kutua katika viwanja vya Tanzania, hatua itakayoongeza abiria, lakini pia hatua hiyo ni kukidhi vigezo vya kimataifa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.