Mahakama EACJ yaitaka serikali kujibu hoja za wapinzani

Mahakama EACJ yaitaka serikali kujibu hoja za wapinzani

20 June 2019 Thursday 09:29
Mahakama EACJ yaitaka serikali kujibu hoja za wapinzani


Na mwandishi wetu, Arusha
MAHAKAMA ya Afrika Mashariki(EACJ) imeitaka serikali ya Tanzania kujibu hoja za upinzani kuhusu kupinga utekelezaji wa baadhi ya vifungu vya sheria mpya ya vyama vya siasa vinavyodaiwa kukiukwa. 
Kiongozi wa jopo la majaji watano wanayoisikiliza kesi hiyo, jaji Monica Mugenyi amesema kutokana na unyeti  wa shauri la wapinzani, ni muhimu kwa serikali kushirikishwa kujibu hoja.

''Hoja za kupinga vifungu vya sheria hii zinapaswa kufikishwa haraka iwezekanavyo upande wa serikali  hii ni kutokana na unyeti wake ili zijibiwe na baadaye mahakama itatoa uamuzi,'' amesema jaji huyo

Jopo hilo Juni 19, 2019 lilisikiliza kwa mara ya kwanza maombi madogo na 2/2019 yanayotokana na shauri na 3/2019 lililofunguliwa hapo kupinga sheria ya vyama vya siasa na 1 ya mwaka 2019.
Washtaki wanaiomba  mahakama ya EAC isimamishe matumizi ya sheria hiyo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.

Walalamikaji katika shauri hilo ni muungano wa vyama nane vya kisiasa wakiwakilishwa na Freeman Mbowe, Maalim Seif Sharif Hamad, Zitto Kabwe na Salum Mwalimu kupitia maombi yao wanaiomba mahakama hiyo izuie sheria hiyo kwa muda hadi shauri namba 3/2019 litakapoamriwa, kwa sababu utekelezaji wake unaendelea kuwaathiri.

Majaji waliosikiliza kesi hiyo ni  Jaji Fakihi Jundu(Tanzania), Charles Nyachai(Kenya), Monica Mugenyi(Uganda), Faustine Ntezilyago(Rwanda) na Charles Nyawelo(Sudani Kusini)

Walalamikaji wanawakilishwa na mawakili Fatma Karume, Mpale Mpoki, Jebra  Kambole na John Mallya

Updated: 21.06.2019 09:59
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.