Mahakama kuu 'yakataa' kufuta hukumu ya kifo

Mahakama kuu 'yakataa' kufuta hukumu ya kifo

19 July 2019 Friday 05:04
Mahakama kuu 'yakataa' kufuta hukumu ya kifo

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa hukumu ya kifo ni kinyume na katiba ya nchi.

Watetezi wa haki za binadamu walifungua kesi kutaka adhabu hiyo ifutwe kwani inakiuka haki ya msingi ya kuishi. Hukumu hiyo haijatekelezwa tangu mwaka 1994.

Wafungwa 500 wanakabiliwa na adhabu ya kifo au kifungo cha maisha.

Baada ya kuahirishwa kwa mara mbili mfululizo hatimaye Julai 18, 2019 majaji wa mahakama hiyo walitoa uamuzi wao kuhusu kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini wakitaka hukumu ya kifo ifutiliwe mbali.

Hukumu hiyo iliyosomwa na jaji Benhajj Masoud imeeleza kwamba hukumu ya kifo itaendelea kuwepo kwa sababu ipo kikatiba

''Hatujaridhika na maamuzi na tutaenda mbele kwasababu ni suala ambalo kidogo limekosa uelewa mzuri kujibu tofauti ya kupinga adhabu ya kifo na na kupinga adhabu ya lazima yakifo'', amesema wakili Fulgence Masawe.

Masawe ambaye alikuwa anaiwakilisha kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC) amesema adhabu ya lazima ya kifo inayotolewa katika kifungu cha 197 inasema ukishapatikana na hatia ya kosa la mauaji, jaji au yeyote aliyekusikiliza hana adhabu nyingine na iliyobaki ni adhabu ya kifo tu.

Anasema katika nchi ambazo zimeendelea anaruhusa ya kuingilia kati kutafuta suluhisho kwa kufanya utetezi maanake mwisho wa siku yule ambaye amepatikana na hatia atapewa adhabu nyingine yoyote mbadala kulinganana na mazingira ya mauaji na kosa alililofanya kwasababu makosa yote hayafanani.

''Ukisoma hukumu nyingi za mahakama kuu tumeona majaji wanalalamika wanapomtia mtu hatiani kwenye kesi ya mauaji wanasema mkono wetu umefungwa, hatuna namna nyingine zaidi ya kutoa adhabu ya kifo'' alisema wakili huyo.

Aidha wakili Fulgence Masawe anapendekeza majaji wapewe uhuru kutoa hukumu kutokana na kesi iliyo mbele yao.

Sasa uenda LHRC ikakata rufaa Mambo  katika mahakama ya rufani.

Mara ya mwisho kwa mfungwa kunyongwa ilikuwa mwaka 1994, enzi za utawala wa Rais wa awamu ya pili wa nchi hiyo, Ally Hassan Mwinyi.

Baada ya Mwinyi akaja rais Benjamin Mkapa ambaye akamwachia kijiti Jakaya Mrisho Kikwete na wote hao hawakusaini mfungwa yeyote kunyongwa.

Mwaka 2017, Magufuli akiwa anamuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma alivunja ukimya juu ya suala hilo.

BBC

Updated: 19.07.2019 06:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.