Mahakama yamuonya Wema Sepetu

Mahakama yamuonya Wema Sepetu

24 June 2019 Monday 15:23
Mahakama yamuonya Wema Sepetu

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

BAADA kutumikia kifungo cha siku saba jela, msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameonywa na mahakama kuwa haitasita tena kumfutia dhamana endapo atakiuka tena masharti

Onyo hilo limetolewa leo Juni 24, 2019 na hakimu mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Maira Kasonde.

Mlimbwende huyo amepewa dhamana na kesi yake itaanza kusikilizwa ushahidi Julai 4, 2019

Juni 17, 2019 Wema alipelekwa katika gereza la Segerea Tabata jijini Dar es Salaam na kutumikia kifungo cha siku saba jela kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Juni 11, 2019  mahakama hiyo ilifuta dhamana na  iliagiza Wema atafutwe mahala popote alipo kutokana na kutofika mahakamani kuhudhuria kesi inayomkabili

Wema ambaye aliwahi kuwa mlimbwende  'miss' Tanzania mwaka 2006 anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani kinyume cha sheria.

Updated: 24.06.2019 16:32
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.