Mahakama yatengua hukumu kifungo cha mbunge Sugu

Mahakama yatengua hukumu kifungo cha mbunge Sugu

11 October 2019 Friday 17:10
Mahakama yatengua hukumu kifungo cha mbunge Sugu

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya imetengua hukumu, Mwenendo na Kifungo alichohukumiwa Mbunge wa Mbeya Mjini(Chadema),Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Leo Oktoba 11, 2019 Jaji John Utamwa alitengua hukumu ya kifungo cha miezi mitano alichohukumiwa na kukitumikia chote Sugu kwa ubatili wa mwenendo katika kesi hiyo.

Akisoma Uamuzi wa Rufaa Namba 29 ya Mwaka 2018 iliyowasilishwa na Sugu kupitia Mawakili Peter Kibatala na Faraji Mangula,Jaji Utamwa amesema kulikuwa na makosa yasiyotibika katika mwenendo wa shauri hilo.

Hasa pale ambapo aliyekuwa Hakimu Mwandamizi Mteite wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya aliposhindwa kuwasomea mashtaka washtakiwa katika hatua ya usikilizaji wa awali (Preliminary Hearing).

Katika Hukumu yake iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Jaji Utamwa amesema hakubaliani na hoja za upande wa Serikali ambao ni wajibu rufaa kwamba mapungufu hayo yanatibika.

Na badala yake Jaji Utamwa amesema makosa hayo yanaathiri mwenendo mzima wa kesi iliyopelekea kufungwa kwa Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga.

Hivyo Jaji Utamwa alitengua Hukumu, Mwenendo mzima wa kesi na adhabu ya kifungo waliyohukumiwa Sugu na Masonga.

Februari 26, 2018 Mbunge huyo wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja baada ya kukutwa na hatia kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.

Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, Maiko Mteite baada ya kuridhika ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.

Pia Mahakama hiyo ilimuhukumu kifungo cha miezi sita katibu wa Chadema kanda ya nyasa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.