Mahakama yawahukumu askari sita

Mahakama yawahukumu askari sita

05 October 2019 Saturday 06:52
Mahakama yawahukumu askari sita

Na mwandishi wetu,Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu askari sita akiwemo Mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kulipa faini ya Sh500,000 kila mmoja bada ya kukiri shtaka la wizi wa mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik).

Waliohukumiwa ni PC Simon (28), PC Dickson, PC Hamza, Koplo Shwahiba(38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ na PC Elidaima Paranjo (38),

Hukumu hiyo imetolewa Oktoba 4, 2019 na Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo baada ya washtakiwa kukiri shtaka linalowakabili

Mwaikambo amesema kwa kuwa washtakiwa hao ni kosa Lao la kwanza hivyo mahakama hiyo imewapa adhabu ya kulipa faini ya Sh500, 000 kila mmoja na kulipa thamani ya zaidi ya milioni 4 ya mafuta ya ndege yaliyoibiwa na madumu 109 yenye mafuta hayo yatarudishwa serikalini.

Awali wakili wa Serikali Mwandamizi Renatus Mkude aliieleza mahakama hiyo kuwa kuna utaratibu wamekubaliana ili kumaliza shauri hilo.

Alidai awali wastakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu na walikubaliana kuliondoa shtaka la kwanza la kupanga genge la uhalifu. Shtaka la pili lilikuwa ni wizi na la tatu ni la utakatishaji wa fedha.

Inadaiwa kuwa Julai 30,2019 katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere uliopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik) yenye thamani ya Sh 4,647,760 mali ya ATCL ambayo waliyaweka kwenye madumu 109. Wote wamekiri kufanya tukio hilo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.