Majambazi matatu yauwawa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea kuwasaka majambazi wawili waliokimbia.

Majambazi matatu yauwawa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea kuwasaka majambazi wawili waliokimbia.

27 May 2019 Monday 15:28
Majambazi matatu yauwawa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUUWAWA KWA MAJAMBAZI WATATU, KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI BASTOLA AINA YA BROWNING NA RISASI TATU.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam mnamo tarehe 25/05/ 2019 majira ya saa nane usiku huko maeneo ya Kigogo Fresh Mtaa wa Seremala jeshi la polisi  lilifanikiwa kuwaua majambazi watatu akiwemo mwanamke mmoja na kisha kukamata bastola mbili aina ya Browning zilizofutwa namba na risasi tatu .


Awali jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam lilipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna kikundi cha majambazi wapatao watano wamepanga kuvamia nyumba ya Bwana ALLY DASTAN (66), Mkazi wa Kigogo Fresh ambaye mke wake aitwaye MOSHI SAID(56) ni Mwenyekiti na ni mtunza hazina  wa Kikundi cha Umoja Group.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kikosi kazi Maalum cha kupambana na ujambazi kiliweka mtego katika nyumba  ya Bwana ALLY na ilipofika majira ya saa nane usiku majambazi hao wapatao watano walivamia nyumba hiyo na baada ya kugundua kuwa kuna mtego wa polisi walianza kurusha risasi na ndipo askari wakajibu mapigo na kufanikiwa kuwajerui majambazi watatu akiwemo mwanamke mmoja na majambazi wawili walikimbia. Majambazi hao walifariki dunia wakiwa njiani wakipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea kuwasaka majambazi wawili waliokimbia.


KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUANZIA TAREHE 01.05.2019 HADI TAREHE 26.05.2019 CHATOZA TOZO TSH 926,310,000/=
Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake  cha Usalama barabarani kinaendelea na oparesheni ya ukamataji wa makosa ya Usalama  Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 01.05.2019 hadi tarehe 26.O5.2019 ni kama ifuatavyo:-
1. Idadi ya magari yaliyokamatwa                   - 24,261
2. Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa                   - 533
3. Daladala zilizokamatwa                           -13,528
4. Magari mengine (binafsi na malori)                   -10,733
5. Bodaboda waliofikishwa Mahakamani
kwa makosa ya kutovaa helmet na kupakia mishikaki  -39
Jumla ya Makosa yaliyokamatwa                             - 27,318      
JUMLA ya Fedha za Tozo zilizopatikana             –  926,310,000/=


Aidha oparesheni ya ukamataji wa magari yanayodaiwa tozo kwa mfumo wa kielektroniki kwa kutumia kamera ni endelevu hivyo madereva wanatakiwa kuwa na leseni zao, wakati wote kwa ajili ya ukaguzi.
Pia madereva, waendesha pikipiki, wamiliki wa magari, pikipiki pamoja na watumiaji wote wa barabara wanatakiwa kutii sheria na usalama barabarani wanatakiwa kutii sheria za usalama barabarani ili kupambana na ajali za barabarani zinazoweza kuzuilika.
Aidha katika kipindi hicho jumla ya magari 11,022 yaliyokuwa hayajalipa tozo kwa wakati yalikamatwa ambapo kiasi kiasi cha Tsh 868,243,500/= zilikusanywa. 
Madereva na wamiliki wote wa magari wanatakiwa  kulipa tozo walizoandikiwa kwa mfumo wa kielektroniki kwa wakati na kwa hiari ili kuepuka kukamatwa na kulazimishwa kulipa tozo hizo.

 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.