Majambazi wanne wauawa kwa kupigwa risasi

Majambazi wanne wauawa kwa kupigwa risasi

12 July 2019 Friday 09:32
Majambazi wanne wauawa kwa kupigwa risasi

Na mwandishi wetu, Pwani.
MAJAMBAZI wanne wamefariki dunia kwa kupigwa risasi kufuatia majibizano ya kurushina risasi  za moto na polisi huku wengine wawili wakitoroka kwa gari.

Tukio hilo limetokea eneo la Kwala, Mlandizi mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa amesema, tukio hilo limetokea Julai 11, 2019 majira ya saa 8 mchana baada ya taarifa kulifikia jeshi hilo kuwapo kwa watu waliopanga njama za kuvamia na kupora fedha za kuwalipa wanaojenga Bandari Kavu ya Kwala.

“Ndipo Jeshi la Polisi tuliweka mtego na majambazi hao kujikuta wakinasa na kuanzisha majibizano ya risasi na kupelekea majambazi wanne kati ya sita waliokuwepo eneo hilo kupoteza maisha,” amesema Wankyo.

Amesema majambazi wawili walitoweka eneo la tukio kwa kutumia gari lingine na msako wa kuwatafuta unaendelea.

Katika tukio hilo majambazi hao wamekutwa na bunduki mbili aina ya pump action, radio call moja, hirizi, dawa za kupulizia watu, kamba za kufungia watu na, plasta za kuziba watu midomoni.

Vitu vingine ni leseni za udereva, vitambulisho mbalimbali vya uraia, kadi ya bima ya afya, koti, kaniki, kanzu, suruali na kaptula.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya mkoa ya Tumbi .

Updated: 12.07.2019 09:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.