Malinzi, wenzake wapunguziwa mashtaka, mmoja aachiwa huru

Malinzi, wenzake wapunguziwa mashtaka, mmoja aachiwa huru

23 July 2019 Tuesday 15:15
Malinzi, wenzake wapunguziwa mashtaka, mmoja aachiwa huru

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imefuta mashtaka 10 kati ya 30 yaliyokuwa yakimkabili aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi na wenzake watatu.

Pia imemuachia huru mshtakiwa wa tano Miriam  Zayumba  baada ya kuonekana  hana kesi ya kujibu kwa mashtaka yote yaliyokuwa yakimkabili.

Malinzi na wenzake  aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya wamebakiwa na mashtaka 20 wanayotakiwa kujitetea. 

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne Julai 23, 2019 na  Hakimu Mkazi, Maira Kasonde baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa na Jamhuri.

Hakimu Kasonde amesema mashtaka ambayo washtakiwa wameonakana hawana kesi ya kujibu, upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kama washtakiwa wana kesi ya kujitetea.

Mahakama iliwafahamisha haki zao washtakiwa kwamba wanaruhusiwa kujitetea wenyewe kwa kiapo ama kuita mtu yoyote kama mashahidi wao.

Pia walifahamishwa kwamba wanayohaki ya kunyamaza kimya lakini kwa kufanya hivyo mahakama itaamini kwamba ushahidi uliotolewa na Jamhuri ni sahihi.

Washtakiwa walikubali kujitetea kwa kiapo na watakuwa na mashahidi ambapo wataanza kujitetea Agosti 6 mwaka huu.

Washtakiwa hao kwa  pamoja wanakabiliwa na mashitaka 20 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017. Ambapo Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba ameachiwa huru.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.

Updated: 24.07.2019 08:56
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.