Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumkata na kisu shingoni

Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumkata na kisu shingoni

16 September 2019 Monday 18:25
Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumkata na kisu shingoni

Na mwandishi wetu, Kilimanjaro

JESHI la polisi linamshikilia mwanamke Philipina Donath(37) mkazi wa kijiji cha Katangara wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro akidaiwa kumuua mwanaye wa kumzaa mwenye miaka mitano kwa kimkata na kisu shingoni .

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Hamis Issah amesema mtuhumiwa amejisalimisha mwenye katika kituo cha polisi na kwamba mauaji hayo yametokea jana Septemba 15, 2019 katika kijiji cha Katangara Mashati.

‘‘Baada ya kumuua mwanaye, mtuhumiwa alijipeleka mwenyewe katika kituo cha polisi Mashati na polisi walipokwenda nyumbani walikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa chini na pembeni kuna kisu kikiwa na damu,’’ amesema kamanda huyo

Kamanda Issah amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Huruma kwa ajili ya taratibu za maziko

Updated: 16.09.2019 18:52
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.