Mamilioni ya sadaka yaibwa Dar

Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na tukio hilo

Mamilioni ya sadaka yaibwa Dar

Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na tukio hilo

05 April 2018 Thursday 14:19
Mamilioni ya sadaka yaibwa Dar

Sio jambo la kawaida kwa watu hata kama wanakabiliwa na ugumu wa maisha kwa kiasi gani kuingiwa na tamaa kiasi cha kuamua kwenda kuiba katika sehemu ya ibada.

Kuna ambao wanaogopa adhabu ambayo huenda wakakabiliwa nayo kutoka kwa muumba wao kufanya uhalifu wa aina hiyo.

Huenda ikawa ndiyo sababu ambayo huyafanya makanisa na misikiti nchini na mahali popote duniani kuachwa wazi, huku vyombo vya thamani vikionekana wazi bila kuwa na mtu ambaye anavilinda.

Lakini inavyoonekana, ni kwamba hali si shwari Dar es Salaam.

Hali iliyowafanya watu, bila kujali nini kinaweza kuwapata kuamua kwenda kufanya uhalifu katika kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, Mbezi jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Aprili 5, 2018 na kupora fedha pamoja na vifaa kadhaa vya kuendeshea misa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo watu hao waliingia kanisani hapo na kuiba vitu hivyo, ikiwemo fedha za sadaka zilizokusanywa tangu sikukuu za pasaka mpaka sasa.

“Ni kweli nimepokea simu kuwa kuna hilo tukio, ni vibaka wameingia hapo kanisani na kuiba pesa na baadhi ya vitu, pesa ambazo zilikuwa za sadaka tangu sikukuu, ila thamani yake bado hatujaijua kwa sababu ndio tukio limeripotiwa sasa, baada ya muda nitakuwa na taarifa kamili”, amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na tukio hilo, ili kuwafikisha mbele ya sharia.

Taarifa zaidi zinasema kuwa wezi hao waliingia kanisani hapo majira ya saa tisa usiku na kuwapiga walinzi wanne wanaolinda kanisa hilo, kisha kuingia chumba maalum kinachoitwa sakristia na kuiba vikombe maalum vinavyotumika kwenye ibada, na pesa taslim takriban milioni nane ambazo zilikuwa za makusanyo ya sadaka katika ibada ya siku ya Pasaka.

Azania Post

Updated: 05.04.2018 14:38
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.