Maria Nyerere atua nchini apelekwa hospitali

Maria Nyerere atua nchini apelekwa hospitali

06 June 2019 Thursday 07:30
Maria Nyerere atua nchini apelekwa hospitali

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MKE wa rais wa zamani wa Tanzania Maria Nyerere amewasili jijini Dar es Salaam Tanzania na kupelekwa hospitalini baada ya kupata matatizo ya kiafya nchini Uganda.

Akizungumza  mtoto wake wa  kiume Makongoro Nyerere amesema kuwa kufuatia matatizo ya kiafya aliyoyapata akiwa jijini Kampala, Madaktari wa Tanzania  walichukua jukumu la kumpatia matibabu kabla ya kumruhusu kurejea nchini Tanzania .

"Tunavyoongea sasa, ndio amewasili Dar es Salaam, na kulingana na mapendekezo kutoka kwa madaktari , tunampeleka moja kwa moja hospitalini kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kuchukua maamuzi yoyote ," alisema Makongoro.

Amesema wanakwenda hospitalini kupata uhakika juu ya ikiwa bado anahitaji kuendela kupata matibabu au yuko katika hali nzuri ya kumuwezesha kurejea nyumbani.

Awali mke huyo wa rais wa zamani wa Tanzania Maria Nyerere alisindikizwa lna maafisa wa Uganda ambako walipandisha ndege kurejea nyumbani baada ya kuugulia nchini Uganda.

Aliondoka kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe kwa ndege rasmi aliyopewa na rais wa Uganda Yoweri Museveni hadi mjini Dar es salaam

Rais Museveni anaripotiwa kutohudhuria sherehe za siku ya mashahidi wa Uganda katika eneo la Namugongo kwa ajili ya kumtembelea Mama Maria mjini Kampala katika  moja ya hospitali mjini humo.

The Citizen

Updated: 09.06.2019 14:21
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.