Mauaji ya watanzania 9 Msumbiji, wanne mbaroni

Mauaji ya watanzania 9 Msumbiji, wanne mbaroni

15 July 2019 Monday 15:49
Mauaji ya watanzania 9 Msumbiji, wanne mbaroni

Na mwandishi wetu, Geita
MKUU wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema polisi inawashikilia watuhumiwa wanne wanaohusishwa na mauaji ya watanzania 9 yaliyotokea  Msumbiji

Juni 29, 2019 IGP Sirro alitoa taarifa ya kuuawa kwa kupigwa risasi kwa watanzania hao na wengine 6 kujeruhiwa nchini Msumbiji ambako walikwenda kujitafutia riziki.

Amesema hayo leo Julai 15, 2019 mkoani Geita katika  uzinduzi  wa nyumba 15 za makazi ya Askari wa Jeshi la Polisi  katika eneo la Magogo Mkoani humo ambazo zitakuwa na uwezo wa kutumiwa na Askari 30.

"Tayari tunawashikilia watuhumiwa watano japo mmoja amefariki lakini wanaendelea kutajana. Taarifa ni kwamba mipango yote ilipangwa Tanzania na utekelezaji ukafanyika Msumbiji,'' amesema Sirro
 
Juni 29, 2019 akiwa mkoani Mtwara eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji, Sirro alisema mauaji hayo yalifanyika Juni 26, 2019 ambapo pia watu wa Msumbuji kadhaa nao waliuawa.

''Waliofanya haya matukio tutawatafuta na nimeongea na IGP mwenzangu wa Msumbiji nimemuomba tukutane kesho Juni 30, 2019 ili tuongee juu ya tukio hili na mengine'', alisema.

IGP Sirro alisema alisikitishwa sana na vifo vya watanzania hao ambao wamepigwa risasi na watatumia kila njia kuwapata waliofanya mauaji hayo.

Imeelezwa kuwa watanzania hao huenda nchini Msumbiji wakati wa msimu wa kilimo kwa ajili ya kulima na kujipatia mazao pamoja na kipato.

Updated: 15.07.2019 15:54
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.