Maziko ya Mugabe yaibua utata

Maziko ya Mugabe yaibua utata

09 September 2019 Monday 14:09
Maziko ya Mugabe yaibua utata

HARARE, Zimbabwe

MWILI wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe unatarajiwa kuwasili Jumatano nchini Zimbabwe na serikali imethibitisha kuwa mazishi yake yatafanyika katika siku mbili za wikendi ijayo.

Mugabe alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, akiwa hospitalini Singapore wiki iliyopita

Lakini sasa inaonekana kuna mzozo wa kutoelewana baina ya familia ya marehemu Mugabe na serikali ya Zimbabwe kuhusu ni wapi kiongozi huyo aliyeitawala Zimbabwe kwa miaka 37 kuanzia 1980 hadi 2017, anapaswa kuzikwa.

Baadhi ya ndugu zake wanataka azikwe katika kijijini alikozaliwa cha Kutama kilichopo katika jimbo la magharibi la Mashonaland yapata kilomita 80 au maili 50 magharibi mwa mji mkuu Harare.

Wengi miongoni mwa mashujaa wa taifa la Zimbabwe - wale ambao walishirikiana katika mapambano dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache wamezikwa katika eneo la makaburi ya Mashujaa lililopo nje kidogo tu ya mji mkuu Harare.

Ndani ya lango la nyumba ya Mugabe ya kijijini kwao , ambayo kwa sasa inalindwa na mlinzi mmoja, makumi kadhaa ya waombolezaji walikusanyika Jumapili kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Mugabe.

Waliketi kwenye makundi madogo madogo, huku wakiongea kwa sauti ya chini. Kulikuwa na hali ya wasi wasi - kuashiria kuwa mambo yalikuwa sio mazuri.

Katika mojawapo ya vyumba vya nyumba hiyo, wazee wa kijiji, na machifu walikuwa wakiamua ni wapi Mugabe angezikwa.

Leo Septemba 9, 2019 Mpwa wake , Mugabe, amekanusha kuwa kulikuwa na suala la kutoelewana na serikali, lakini akakiri kuwa mjomba wake alikufa akiwa mtu mwenye hasira sana baada ya kung'olewa madarakani mwaka 2017 na jeshi pamoja na makamu wake wa zamani.

"Alikuwa mwenye machungu ...Unaweza kufikiria watu ambao uliwaamini- watu ambao walikuwa wakikulinda,wakikushughulikia, usalama wako unakugeuka. Alikuwa mwenye masikitiko makubwa na iliweka doa kwenye utawala wake ," alisema

Wakuu wa mataifa mbalimbali wamealikwa katika sherehe za umma za kutoa heshima kwa Mugabe, lakini si kwa ajili ya mazishi halisi

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.