Mbaroni akidaiwa kumuua mkewe kwa kumkata shingoni

Mbaroni akidaiwa kumuua mkewe kwa kumkata shingoni

09 July 2019 Tuesday 12:28
Mbaroni akidaiwa  kumuua mkewe kwa kumkata shingoni

Na mwandishi wetu, Handeni. 
JESHI la polisi mkoani Tanga  linamshikilia Juma Hemedi (45) mkazi wa mtaa wa Kwamaraho kata ya Malezi wilayani Handeni mkoani Tanga, akituhumiwa kumuua mkewe Amina Husein (38) kwa kumkata shingoni.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Edward Bukombe amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema lilitokea usiku wa kuamkia Julai 8 huku chanzo chake ni sababu za kimapenzi ambapo kulikuwa na ugomvi wa kifamilia na polisi wanafuatilia kwa undani zaidi.

"Taarifa za awali zinasema sababu za mauaji hayo ni za kimapenzi, kwamba marehemu na mumewe walikuwa na mgogoro wa kifamilia na sisi kama polisi tunafuatilia kwa undani zaidi ili kupata undani wa tukio hilo," alisema Bukombe.

Diwani kata ya Malezi, Shabani Kitombo akiwa eneo la tukio amelaani kitendo hicho na kusema kuwa inaonyesha mwanamke huyo amekatwa panga eneo la shingoni.

Alisema kitendo hicho ni cha kinyama na haijawahi kutokea hapo kabla katika uongozi wake kwa mwananchi kuuawa kinyama kiasi hicho kwa kuchinjwa shingo.

Jophrey Kisanga mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu alisema wamekuta una jeraha la kukatwa na panga katika upande wa kushoto wa shingo yake.

Updated: 09.07.2019 12:42
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.