Mbowe, wenzake wapewa wiki mbili

Mbowe, wenzake wapewa wiki mbili

21 October 2019 Monday 15:43
Mbowe, wenzake wapewa wiki mbili

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

NOVEMBA 4, 5 na 8, 2019 viongozi tisa wa Chadema akiwemo Freeman Mbowe wataanza kujitetea dhidi ya kesi ya jinai namba 112 ya mwaka 2018 inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba alitoa uamuzi huo mdogo leo Oktoba 21, 2019  mbele ya mawakili wa utetezi,Jeremiah Mtobesya, Hekima Mwasipu na mawakili wa serikali,Faraja Nchimbi, Wankyo Simon na Salim Msemo.

Hakimu Simba akitoa uamizi huo alisema wiki Tatu zilizoombwa na upande wa utetezi ni nyingi hivyo aliwapatia wiki mbili ili waweze kuwaanda washtakiwa waanze kujitetea kabla ya mashahidi wao

Hakimu Simba alisema mashahidi katika kesi hii mbali na washtakiwa ni wengi kweli 200 upande wa utetezi wanahitaji kupewa muda wa maandalizi.

Lakini huo muda wa wiki tatu ulioombwa na upande wa utetezi, mahakama inaona huo muda ni mrefu lakini kwa mazingira ya Kesi hiyo na namba ya mashahidi iliyotwa,aliwapatia muda wa wiki mbili ili waweze kujiandaa na utetezi.

Kuhusu kielelezo namba 5 ambacho ni video ya maandamano kilichoombwa na upande wa utetezi ili wataalam wao wakichunguze kwa sababu wana wasiwasi kimehaririwa, Hakimu Simba alisema

watakitumia kupitia vifaa vya mahakama vile vile vilivyotumiwa na upande wa mashtaka.

Hata hivyo watakuwa chini ya usimamizi wa mtendaji wa mahakama ili kuangalia usalama wa jengo, vielelezo na vifaa vitakavyotumiwa na kwamba upande wa utetezi utoe taarifa kwa mahakama siyo chini ya siku tatu ili maandalizi yafanyike.

"Kutoka na wingi wa mashahidi hakuna namna kusikiliza kesi hii mfululizo na ni lazima isikilizwe mfululizo itaanza Novemba 4,5 na 8, 2019" alisema Hakimu Simba.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Oktoba 18,mwaka huu, Wakili wa utetezi Peter Kibatala kuomba wapatiwe muda wa wiki tatu ili waweze kuandaa washtakiwa na mashahidi wao kwa utetezi.

Awali Kibatala aliieleza mahakama kuwa washtakiwa hao watatoa ushahidi wao chini ya kiapo kwa kadri dini zao zinavyoruhusu.

Washtakiwa hao wanaanza kutoa utetezi wao baada ya mashahidi nane wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao na Mahakama kuwaona washtakiwa hao wana Kesi ya kujibu wajitetee.

Wanaokabiliwa katika kesi hiyo, mbali naMwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Wengine ni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Updated: 21.10.2019 15:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.