Mbunge ataka kamati ndogo kuchunguza mfumo wa TANCIS Zanzibar

TANCIS ni mfumo wa uondoaji mizigo bandarini huko Zanzibar

Mbunge ataka kamati ndogo kuchunguza mfumo wa TANCIS Zanzibar

TANCIS ni mfumo wa uondoaji mizigo bandarini huko Zanzibar

05 June 2018 Tuesday 13:19
Mbunge ataka kamati ndogo kuchunguza mfumo wa TANCIS Zanzibar

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Wingwi kwa tiketi ya chama cha wananchi (CUF) Juma Kombo Hamad ameitaka serikali kuunda kamati ndogo kwenda Zanzibar kuchunguza ukubwa wa tatizo la mfumo wa uondoshaji wa mizigo bandarini unaojulikana kama TANCIS.

Alikuwa akiuliza swali la nyongeza bungeni leo ambapo alisema kuwa kuwepo kwa mfumo huo visiwani Zanzibar kumeleta matatizo makubwa sana miongoni mwa wafanyabiashara.

Alisema kuwa Zanzibar ni kisiwa kidogo chenye watu wasiozidi milioni 1.5 na wafanyabiashara wengi toka nje wanategemea sana kibiashara na hivyo kuwalazimisha kuingia kwenye mfumo huo kumeleta changamoto kubwa na kuitaka serikali kuunda kamati ndogo kwenda huko kulipatia ufumbuzi suala hilo.

Akijibu swali lake, Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji, alisema kuwa kinachokea ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ushindani sawia wa wafanyabiashara.

Alisema kuwa kulikuwa na wafanyabishara wanakwenda Zanzibar kununua bidhaa kwa bei ya chini na kuzileta bara na hivi sasa lazima walipe kodi.

Hata hivyo alibainisha kuwa serikali ya Zanzibar na Tanzania bara zinalifanyia kazi suala hilo na majadiliano yamefikia sehemu nzuri.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Lucy Mlowe (CCM) aliyetaka kujua mpango wa serikali kuhakikisha watumishi walioajiriwa mwaka 1980 ambao hawakukatwa fedha kwenda kwenye mfuko wa PSPF wanapelekewa alisema hakuna kama jambo hilo.

Mbunge huyo alitaka kujua mikakati ya serikali kuhakikisha kuwa fedha hizo zinapelekwa PSPF kwa wakati muafaka.

Akijibu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, alisema kuwa awali watumishi hao walikuwa hawachangii kwenye mifuko, lakini wanastahili kulipwa malipo ya uzeeni.

Alifafanua kuwa watumishi wote wa serikali wanakuwa wananchama wa PSPF wanakuwa wanachama tangu mfuko huo ulipoanzishwa.

Kuhusu kiwango cha chini cha pensheni kwa wastafu kila mwezi alisema kuwa kwa sasa kimepanda na kuwa shilingi laki moja, kutoka shilingi elfu hamsini za awali.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.