Mbunge ataka tai, skafu, bendera viwe vazi la taifa

Mbunge ataka tai, skafu, bendera viwe vazi la taifa

17 June 2019 Monday 10:14
Mbunge ataka tai, skafu, bendera viwe vazi la taifa

Na mwandishi wetu, Dodoma
MBUNGE wa Iramba Magharibi(CCM), Dk Mwigulu Nchemba ametaka vazi la tai, skafu na bendera ya nchi virasimishwe rasmi kuwa vazi la taifa.

Ametoa hoja hiyo alipouliza swali la nyongeza leo Juni 17, 2019 Bungeni Dodoma. Swali la msingi lilikuwa ni lini vazi la taifa litapatikana na kutangazwa rasmi.

Akijibu hoja hiyo, Naibu waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema wizara italifanyia kazi suala hilo.

Akijibu swali la msingi amesema tayari serikali imeshafufua upya mchakato wa  upatikanaji wa vazi la taifa.

"Tumeshafufua mchakato upya wa upatikanaji wa vazi la taifa.  Kuhusu skafu, tai na bendera ya nchi kuwa vazi la taifa hilo tumelipokea,'' amesema 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.