banner58

Mbunge CCM adai sheria zinalinda sana migodi mikubwa kuliko wazawa

Mbunge huyo alisema kuwa kwa hali ilivyosasa inaonekana kuwa sheria zinalinda sana migodi mikubwa kwani wanapendelewa sana

Mbunge CCM adai sheria zinalinda sana migodi mikubwa kuliko wazawa

Mbunge huyo alisema kuwa kwa hali ilivyosasa inaonekana kuwa sheria zinalinda sana migodi mikubwa kwani wanapendelewa sana

01 June 2018 Friday 10:24
Mbunge CCM adai sheria zinalinda sana migodi mikubwa kuliko wazawa

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Geita Mjini Constantine Kanyasu (CCM) amedai kuwa sheria zinaipendelea sana migodi mikubwa kuliko wananchi na hivyo kuongeza uwezekano wa kuleta uhasama zaidi miongoni mwao.

Akizungumza kutoka Dodoma leo asubuhi, Mbunge huyo alisema kuwa kwa hali ilivyosasa inaonekana kuwa sheria zinalinda sana migodi mikubwa kwani wanapendelewa sana.

Akitolea mfano alisema kuwa migodi imepewa maeneo makubwa huku baadhi wananchi wakikosa maeneo ya kufanyia shughuli zao.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya maeneo waliyopewa migodi hiyo huwa haitumiki kwa sana lakini inawekewa ulinzi kuzuia watu wasiingie.

Aliongeza kuwa inapotokea wananchi wanaingia maeneo hayo yasiyotumika hupigwa na kuumizwa jambo linaloweza kuleta uhasama, na kushauri serikali kuangalia kubadilisha uamuzi wake.

Hata hivyo alipendekez kuwasaidia wachimbaji wadogo ili waweze kutumia zana za kisasa na kuweza kuongeza mchango wao kwenye pato la taifa.

Kwa sasa makampuni makubwa ya madini yanachangia asilimia 98 ya pato hilo huku wachimbaji wadogo wakichangia asilimia mbili tu

Kuhusu mazingira, alisema kuwa kuna umuhimu wa kuyalinda hasa yale maeneo ya uchimbaji wa madini.

Alipendekeza kuja na mbinu mbadala kwa mfano ya kutokutumia miti hasa kwa wachimbaji wadogo na kurudisha mfumo wa uoto wa asili.

Alishauri kubadilishwa kwa mifumo yote inayoonekana kuwanufaisha wachache kwenye sekta ya madini.

Hata hivyo alipongeza juhudi za serikali  ilizoonyesha katika kusimamia sekta ya madini ikiwemo ujenzi wa ukuta wa Mererani kule mkoani Manyara kwa ajili ya udhibiti wa madini ya Tanzanite.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.